BANDA MEDIA BLOG

No title

WAKILI AVITAKA VYAMA VYA KIRAIA KUWA NA UELEWA WA KAZI WANAZOFANYA KWENYE JAMII …..!!!!!!!

Makamu wa rais, wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Deus Nyabiri akizungumza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari, nje ya katika hotel ya Rafiki jijini Dodoma, mara baada ya kufungua kongamano hilo

Mshauri Mwelekezi wa maswala ya maendeleo,  Sia Ngowo Akifafanua jambo wakati alipokuwa akitoa Mada katika Kongamano hilo..

            Sehemu ya Washiriki wa Kongamano hilo lililozihusisha Asasi zisizo za kiserikali
                     Sehemu ya Washiriki wa Kongamano hilo lililozihusisha Asasi zisizo za kiserikali
             Sehemu ya Washiriki wa Kongamano hilo lililozihusisha Asasi zisizo za kiserikali
                             Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakijitambulisha
                          Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakijitambulisha
                       Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakijitambulisha

                             Washiriki wakinyoosha viungo wakati wa Kongamano hilo




                 Wakili Mary Munis akizungumza jambo kwenye Kongamano hilo
  Ofisa Programu kutoka Jukwaa la Katiba Tanzania, (JUKATA) Thobias akizungumza na vyombo vya habari

              ....................................................................

        NA JOHN BANDA, DODOMA            

MAKAMU wa rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Deus Nyabiri amezitaka asasi za kiraia kuwa na uelewa wa kazi wanazozifanya kwenye Jamii.

Pia imeelezwa kuwa matukio ya ‘unyanyasaji’ dhidi ya watendaji wa mashirika ya kiraia yamepungua kwa kiasi kikubwa kati ya 2021 na 2023.

Nyabiri Amesema hayo December 12,2023 wakati akifungua semina ya kuzijengea uwezo asasi za kiraia kuhusiana na masuala ya utawala bora iliyoandaliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa asasi za kiraia kuelewa wanachokifanya ili kuelimisha Jamii kwani wao ni kiungo muhimu kati ya wananchi na Serikali.

“ Sasa tunakaribia kwenda kwenye uchaguzi je asasi zinajua mambo yanayohusiana na uchaguzi? zinajua sheria, kanuni za uchaguzi, mabadiliko yanayotokea, ,?, ” amesema na kuhoji

Wakali huyo Amesema, kuna haja kwa kila asasi kujua wajibu wake, ili kuweza kutekeleza mipango na miradi yao kwa ufanisi, kwa maslahi yao, serikali na wananchi.

Amesema ni vyema kwa kila asasi za kiraia, zikawa na ubobezi kwa kile wanachokitekeleza, ili kuwe na ufanisi wa kuleta mabadiliko kwenye jamii na taifa kwa ujumla..

Kwa upande wake, Mshauri Mwelekezi wa masuala ya maendeleo, sekta ya Asasi za Kiraia (AZAKi), Sia Ngowo Amesema utafiti wa msingi juu ya mazingira ya Sera ya Kisheria kwa Ushirikishwaji wa AZAKi, katika Utawala wa Kidemokrasia ulifanyika Tanzania Bara na Zanzibar (Mei na Juni 2023).

Ngowo Amesema kuwa lengo la utafiti huo lilikuwa ni kukusanya taarifa za msingi kuhusu sheria, sera, na fursa za kiutendaji na changamoto za ushiriki wa AZAKi katika utawala wa kidemokrasia.

 

Amesema jumla ya watu 311 walishiriki huku asilimia 44.6wakiwa wanawake, taasisi zaidi ya 60 pia Wadau wengine walijumuisha maofisa wa umma na wawakilishi kutoka sekta binafsi (vyombo vya habari na mashirika ya kisheria).

Amesema katika utafiti huo, walibaini kuwa AZAKi zinakabiliwa na changamoto katika kutekeleza utetezi unaozingatia ushahidi.

Pia upatikanaji wa nyenzo muhimu kwenye nafasi ya kiraia ni mdogo kwa asilimia 46, asilimia chini ya tano ya AZAKi zinafanya tafiti kuhusu hali ya maeneo ya kiraia.

“Ripoti za kina za hali kuhusu wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu hazipo kabisa,” amesema.

Aidha amesema asilimia 70 ya AZAKi zinakabiliwa na matatizo ya kifedha, jambo linalozuia uchangamfu na ushiriki wao.

“Ufadhili unazidi kuwa changamoto, huku asilimia 68 ya AZAKi zikipokea ruzuku kutoka kwa mashirika matatu tu ya ndani, kama vile Foundation For Civil Society na LSF,” amesema.

Abainisha kuwa kuna haja ya kuwepo kwa majukwaa rasmi ya ushirikiano kati ya AZAKi na serikali, ikiwa ni pamoja na yale ya kisheria, ambayo yanatoa njia za ushirikiano na mazungumzo.

Akizungumzia hali ya uzingatiaji wa AZAKi, Sia Amesema kuwa asilimia 32, ya AZAKi zilionyesha uelewa wa hali ya juu. Asilimia 56 wana kiwango cha wastani cha ufahamu. Pia uelewa mdogo unaohusishwa zaidi na AZAKi za vijijini - kutokana na upatikanaji mdogo wa habari.

“Pia asilimia 63 ya AZAKi, zimeridhika na mahitaji ya sasa, Kuongezeka kwa ujuzi na usimamizi wa taratibu za kufuata.

Pia asilimia 59, ya AZAKi zilitambua taratibu changamano za kufuata kama suala la msingi, linaloathiri uzingatiaji.Asilimia 35 ya AZAKi zilitambua masuala yanayohusiana na gharama, kama vile ada nyingi, kodi na tozo, kama suala jingine kuu linaloathiri uzingatiaji.

 

Amesema asilimia 8. Tu ya AZAKi zinazohusika katika vikao vya kujenga uwezo ili kuongeza uwezo na uelewa.

Pia AZAKI, za vijijini zinakabiliwa na changamoto za kupata barua pepe kwa wakati.

“Katika kipengele cha Uthabiti wa Mifumo ya Kisheria: Hakuna mabadiliko makubwa ambayo yamefanywa kwenye mifumo ya kisheria, inayoongoza jumuiya za kiraia Tanzania Bara na Zanzibar tangu mwaka 2021,” amesema

Pia amesema kuwa kuna upole unaoonekana katika kutekeleza sheria na kanuni na vifungu 'kandamizi'.

“Matukio ya ‘unyanyasaji’ dhidi ya watendaji wa mashirika ya kiraia yamepungua kwa kiasi kikubwa kati ya 2021 na 2023.

Ameweka wazi kuwa mikataba muhimu, kama vile CAT, Itifaki ya Afrika ya Uchaguzi na Demokrasia, na Itifaki ya Walemavu, haijaidhinishwa na kupitishwa nchini hadi 2023.

“Asilimia 44 ya AZAKi mara nyingi hushirikiana na serikali katika shughuli zao., pia asilimia 42 ya AZAKi wakati mwingine hushirikiana na serikali. asilimia 8 ya AZAKi hushiriki mara chache, wakati asilimia 4 hawajihusishi na serikali,” amesema

 Pia ameongeza takribani asilimia tano tu ya AZAKi zilizo na hati iliyoandikwa ya mkakati wa ushiriki wa washikadau/ubia. na asilimia 46 ya AZAKi mara nyingi hushiriki katika mikutano ya kawaida na serikali, asilimia 31 mara nyingi hushiriki katika mashauriano ya kiufundi,

asilimia 30 mara nyingi hujihusisha na majukumu ya uangalizi wa kawaida, kama vile ufuatiliaji na serikali.

Asilimia 19 mara nyingi hushirikiana na serikali katika kuunda uingiliaji wa pamoja.

Naye Ofisa Programu kutoka Jukwaa la Katiba Tanzania, (JUKATA) Thobias amesema kuwa wapo tayari kutoa mapendekezo juu ya mabadiliko ya sheria ya Asasi za kiraia ambayo inataka kila baada ya miaka 10, kusajiliwa upya kwani hilo litaleta migongano kati yao na wafadhili.

 

Pia aliishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwaunganisha na serikali.

mwisho


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG