BANDA MEDIA BLOG

No title

 WANAWACHAMA WA DOWOSA WATAKIWA KUWA WASTAARABU NA WAVUMILIVU ILI MALENGO KUSUDIWA YAWEZE KUFIKIWA


   Wajumbe wa Bodi Hiyo ni Mwenyekiti Kituina Kippa, Makamo Mwenyekiti Justina Mashiba pamoja na Tumaini Sanga, Penina Mnyaki na Elizabert Kasimika ambao ni wajumbe, huku kamati ya Usimamizi Anjelina Sanga, Grace Chigongolo na Mary Mabaya.  


                                                                    Kura zikipigwa

                                                                   Mkutano ukiendelea
                                                     Sehemu ya Wajumbe wa mkutano huo





                  ..............................................

                            NA MWANDISHI WETU,

                            BANDA MEDIA ONE.COM,DODOMA

 MWENYEKITI mteule wa chama cha Ushirika na Mikopo cha DODOMA Woman Saccos, (DOWOSA) Kituwina Kipa amesema ili chama hicho kiweze kutimiza malengo kusudiwa inabidi wanachama wake wawe wastaarabu na wenye kupenda ushirikiano.

 “ili Saccos hii iweze kutimiza Malengo yaliyokusudiwa ya kumkomboa mwanamke kiuchumi inabidi  kuacha uswahili, kuwa wavumilivu, wapende kushirikiana na kuzingatia ustaarabu”, amesema

  Kipa ameyasema hayo wakati alipokuwa akifunga mutano wa Uchaguzi wa viongozi wa DOWOSA uliofanyika Desenba 21,2023 jijini Dodoma ambapo wanachama waliwachagua wajumbe wa Bodi na kamati ya Usimamizi.

 amesema hakuna mtu anayetamani kufanya vibaya, Tusilete Uswahili bali Uswahili tuuache huko mitaani maana sisi sote ni wastaarabu na tunataka maendeleo kupitia saccos yetu’’,

 Aidha amesema baada ya Uchaguzi huo kukamilika sasa kazi za Saccos Zinaanza Rasmi na hivyo kuwataka wanachama wote kumalizia kununua Hisa ili waweze Kukopesheka

 “kila mtu amepita pale nje ameona jina lake na kiasi cha hisa alizonunua, niombe kama tulivyokubaliana kila mtu anunue hisa 10 ambazo ni tsh. 100,000 Laki moja na pia aweke Akiba yake ili iwe rahisi kukopeshwa.

 Awali Mgeni Mualikwa Asha Towfik ambaye ni Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Dodoma, amesema Saccos Hiyo itawakomboa wanawake kuondokana na mikopo ya kausha Damu ambayo  imepelekea machafuko na kuvunjika kwa ndoa za baadhi ya wanawake waliojihusisha na Mikopo hiyo, kutokana na liba kubwa ambapo DOWASA Itatoza asilimia moja peke .

 Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Bodi Hiyo ni Mwenyekiti Kituina Kipa, Makamo Mwenyekiti Justina Mashiba pamoja na Tumaini Sanga, Penina Mnyaki na Elizabert Kasimika ambao ni wajumbe, huku kamati ya Usimamizi Anjelina Sanga, Grace Chigongolo na Mary Mabaya.  

 

 

 

 

 

 

 

 


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG