BANDA MEDIA BLOG

No title

 WIKI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU YAENDELEA JIJINI DODOMA, HUKU WANANCHI WAKIMIMINIKA KUTAFUTA MSAADA WA KUPATA HAKI ZAO ZA ARIDH







                     ...............................................................

NA JOHN BANDA, DODOMA

IMEBAINIKA kuwa migogoro ya Aridh  jijini Dodoma Bado ni Donda Ndugu Kutokana na wananchi walio wengi kuendelea kumiminika katika Mabanda ya maonyesho yanaotoa Elimu mbalimbali ikiwemo haki za Binadamu kupitia umiliki Aridh.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Raisi, Menejimenti ya Utumishi wa UMMA na Utawala Bora, Anayeshuhulikia Ukaguzi na Maadili katika Idara ya Usimamizi wa Maadili, Ally Abdu Ngowo alipoongea na waandishi wa habari, Jijini, Dodoma wakati akiambatana na baadhi ya viongozi wa taasisi simamizi kukagua namna taasisi zilizojitokeza kutoa huduma katika wiki ya maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu yanayoendelea Jijini humo

Ngowo Amesema Uzoefu walioupata baada ya Kumaliza kutembelea Mabanda hayo wamebaini kuwa, Migogoro ya Aridh Bado ni changamoto kubwa jijini humo lakini serikali imeboresha utoaji huduma Kwa kuanzisha Kliniki ya Aridh Kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma

Aidha amesema kuwa Kwa upande Mmoja wananchi wamekuwa wakichangia kusababisha migogoro hiyo kutokana na kuuza mashamba au viwanja zaidi ya mara moja

" Nitoe wito Kwa wananchi kuacha kuuza Aridh zao Kwa mtu zaidi ya mmoja, pia hata upande wa wataalamu wetu wa Aridh  waache kufanya zile (Double Allocation)  ili kuindoa migogoro hiyo", amesema 

Ameongeza kuwa tume hiyo ina Imani ya kuondoa Mianya ya Rushwa, kutokana na Mpango wa uanzishwaji wa Mfumo wa TEHAMA ambao utanyesha wamiliki wa kila kiwania na mashamba.


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG