Zaidi ya nchi 20 zashiriki muungano wa kutoa ulinzi katika Bahari ya Sham, Marekani yasema
Wahouthi wamevamia meli katika njia muhimu ya usafirishaji kama njia ya kuunga mkono Wapalestina Gaza. / Picha: Reuters Archive
Marekani imetangaza kuwa
muungano wa kimataifa wa Bahari ya Shamu Jumatatu, huku siku mbili baadaye,
Wahouthi nao wakionya kwamba watavamia tena ikiwa watashambuliwa.
"Tumekuwa na zaidi ya
mataifa 20 sasa yaliyosaini kushiriki "katika muungano huo, msemaji wa
Pentagon Meja Jenerali Pat Ryder aliwaambia waandishi wa habari Alhamisi.
Vikosi chini ya muungano huo
"vitatumika kama doria ya aina ya barabara kuu, vikizunguka Bahari ya Sham
na Ghuba ya Aden kukabiliana na kusaidia kama inavyohitajika meli za kibiashara
ambazo zinapita njia hiyo muhimu ya maji ya kimataifa," alisema Ryder,
akiwataka Wahouthi kusitisha mashambulizi yao.
Wahouthi wanaoshirikiana na
Iran wamelenga meli mara kwa mara katika njia muhimu ya usafirishaji kwa
kushambulia wakisema wanaunga mkono Wapalestina huko Gaza, kufuatia
mashambulizi ya Israeli yaliyowaua zaidi ya raia 20,000 tangu Oktoba 7.
Onyo la kulipiza kisasi
Israel imeanza mashambulizi ya
mara kwa mara dhidi ya Wapalestina katika eneo la Gaza lililozingirwa baada ya
mashambulizi ya Hamas mnamo Oktoba 7, pamoja na uvamizi wa ardhi unaolenga
maeneo ya raia Kusini na Kaskazini, pamoja na hospitali, kambi za wakimbizi,
shule, na maeneo ya makazi.
Licha ya madai ya Israel ya
kulenga Hamas, mashambulizi ya Israeli yamesababisha kufurushwa kwa angalau
asilimia 85 ya Wapalestina.
Idadi hiyo ni kubwa sana, na
mpaka sasa zaidi ya raia 20,000 wamepoteza maisha na zaidi ya watu 52,600
wamejeruhiwa katika vita hivyo vya siku 77.
Mashambulizi ya Israel, ambayo
bado yanaendelea, yametoa msukumo kwa mashambulizi ya makundi yenye silaha
katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya Houthi dhidi ya
usafirishaji wa Bahari ya
Sham.
