BANDA MEDIA BLOG

DKT, TULIA MGENI RASMI UZINDUZI WIKI YA SHERIA DODOMA

 











PICHA zinaonyesha Tayari Wiki ya Sheria imeanza wananchi na viongoizi mbalimbali wanatembelea mabanda na kupata Elimu Stahiki.

            ............................................................

              NA JOHN BANDA, DODOMA

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Akson Kesho Januiari 27,2024 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa wiki ya sheria katika viwanja vya nyerere square jijini Dodoma

Ambapo kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa  na Mtendaji Mkuu wa Mahakama inaonesha kuwa maadhimisho ya wiki ya sheria inaanza januari 24 hadi 30 mwaka huu ikijumuisha wadau wa haki jinai na taasisi nyingine za serikali na sekta binafsi

Maadhimisho hayo yanayojumuisha taasisi 45, wakiwemo wadau wa haki jinai na taasisi nyingine za kiserikali pamoja na sekta binafsi,kuelekea wiki na siku ya sheria ambayo huadhimishwa februari 1 kila mwaka Dkt. Tulia atashiriki Matembezi ya km. 10

Pamoja na mambo mengine katika uzinduzi huu Dkt.Tulia atazindua Mfumo wa transcription and Translation system(TTS)na baadae kuwahutubia wadau wa sheria haki jinai,watendaji wa Mahakama na wananchi wa ujumla


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG