BANDA MEDIA BLOG

No title

HAKUNA MAENDELEO BILA AMANI_ RAIS DR. MWINYI.




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema hakuna maendeleo pasipo na amani, umoja na mshikamano wa watu.

Rais Alhajj Dkt.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika  ibada ya sala ya Ijumaa  Msikiti wa Riyadhu swalihin Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 05 Januari 2024.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi amewataka waumini kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa ni wajibu kuwanasihi vijana kufanya kazi za halali na kuepuka kushiriki vitendo viovu.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG