JESHI LA POLISI LAWATAKA WAMILIKI WA SHULE KUPELEKA MAGARI YA
KUSAFIRISHIA WANAFUNZI YAKAKAGULIWE.
....................................................................
Na Mwandishi Wetu DODOMA.
BANDA MEDIA
ONE.COM
ILI kuhakikisha Usalama wa wanafunzi kwenye vyombo vya Usafiri Jeshi
la polisi kikosi cha usalama barabarani Jijini Dodoma limekuja na mkakati
maalum wa kuwaandikia barua za wito wamiliki wote wa Shule Binafsi na zile
zinazotumia magari kwa ajili ya kubebea wanafunzi kuyapeleka magari yote
yakakaguliwe
Hayo yamebainishwa hii leo Janualy 4,2024 jijini humo na Koplo Ester Makali kutoka Ofisi
ya Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani Dawati la Elimu kwa UMMA Mkoa wa
Dodoma, wakati akiongea na waandishi wa habari, ambapo amesema Jeshi hilo
limejipanga kuhakikisha Magari yote yanayotoa huduma hiyo yanakuwa na Ubora
Unaotakiwa kuelekea mwaka mpya wa masomo.
Koplo Makali amesema tayari Barua hizo zimeanza kusambazwa kwa
Wamiliki wa Shule hizo na kwamba Magari
yote ambayo hayatakaguliwa hayataruhusiwa Kutoa huduma hiyo Muhimu kwa Watoto.
“Tumewambia wamiliki wote wa shule zinazotumia usafiri wa mabasi
kwa wanafunzi, wahakikishe wanayeleta Magari yote tuyakague kabla ya kukunguliwa
kwa Shule hapo Januali 8, na kila Mmiliki anatakiwa kutii Sherea Bila Shuruti,
na kwamba baada ya hapo tutaendelea kuyakagua kila mara wakati yakiendelea
kubeba watoto,
Tumeamua kufanya hivyo kwa lengo la Kuondokana na ajali zisi za
lazima lakini pia, wakati mwingine magari hayo yanapohalibika hovyo Barabarani
inawafanya watoto kukosa haki yao ya msingi kujaliwa na kupata Elimu sawa na
ratiba ya Shule”, amesema
Ameongeza kuwa Dereva
yoyote atakayekamatwa akiwa amepakia watoto zaidi kwenye Siti moja atachukuliwa
hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini ya makosa ya Barabarani.
Aidha amsema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa Madereva wa Magari
hayo kutokubali kupokea magari mabovu kutoka kwa wamiliki wa shule lakini
wamekuwa wakishindwa kufanya hivyo kwa kigezo cha ugumu wa Maisha kwani
hali hiyo imekuwa ikiwasababishia wao kupata Usumbufu wa kuhalibikiwa
barabarani au kupa ajari.
Baadhi ya Wazazi na Walezi akiwemo Agatha Mataze Mkazi wa Mkoze
Jijini Dodoma wamesema jambo liningine lakuangaliwa ni namna ya kudhibiti
mwendo kasi wa baadhi ya madereva ambao wakati mwingine wamekuwa wakiendesha
magari hayo kama wapo kwenye mashino..
Kutona na Shule kufungwa katika kipindi hiki Juhudi za
kuwatafuta na kuwapata wamiliki wa shule hizo ili watueleze jinsi walivyojipanga zimegonga
mwamba, japo juhudi kuwatafuta zinaendelea…