SPIAKA wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania DKT. Tulia Akson amewashauri Wadau wa Haki jinai
kuhakikisha wanaenda na kasi waliyo nayo mahakama ili kurahisisha utoaji wa
Haki kwa wananchi wanaostahili kuipata
Dkt, Tulia ametoa ushauri huo wakati akizindua
maadhimisho ya Wiki ya Sheria leo Januari 27, 2024 katika viwanja vya Nyerere
Square jijini Dodoma, uzinduzi huo ukitanguliwa na matembezi ya km 10
yaliyowahusisha wadau mbalimbali wa Haki jinai, Taasisi mbalimbali za Serikali,
Sekta Binafsi wakiwemo wananchi wa jiji la Dodoma.
Amesema Mahakama ya Tanzania imeimarisha
Mfumo wa TEHAMA kwa kuanzisha Mfumo wa Akili Bandia kwa Lengo kuharakisha
utoaji wa haki, hivyo kila mdau wa haki jinia wakiwemo Polisi, Magereza,
Takukuru na vyombo vingine vya utoaji haki wahakikishe wanaungana na Mahakama.
“wadau wengine wa haki jinai
tuhakikishe tunaungana na wenzetu ili tukaharakishe kutoa haki kwa wananchi na
yoyote ambaye atasuasua atakuwa akiichelewesha mahakama kutoa haki kwa wakati
kwa yule anayestahili”Amesema
Aidha Spika amempongeza Mtendaji mkuu
wa Mahakama kwa kuja na mfumo wa Akili Bandia kwa ajili ya kurahisisha Utoaji
wa Haki kwa wakati na kuitaka mahakama
kuwa na utayari wa kupokea kesi za watu ambao watalalamika kubambikiwa ushahidi
na Mfumo huo.
Awali
Mtendaji mkuu wa Mahakama Elsante Ole Gabriel amesema mfumo huo wa
unukuzi na tafsiri unatafsiri lugha mbili zinazotumiwa na watanzania ikiwemo
kiswahilki na kiingereza kwa kufuata lafudhi ya makabila ya watanzania ambao
kwa sasa imeshafungwa katika vituo 11 hapa nchini.