BANDA MEDIA BLOG

BAADA YA BUNGE GARLS BUNGE BOYS YANUKIA

 



Wabunge Wakishiriki Shindano la Kula
Mpira wa Pete nao Ukapigwa 

Yanga wakatumia nafasi hiyo kusaji wanachama wapya
Wabunge mashabiki wa Yanga na Simba wakavishwa Medari za Ushiriki




Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Tulia Akson akipokea Tiketi ya Ndege toka kwa Meneja Mauzo wa Shirika la Ndege QATAR AIRWAYS Julieth Mkunyi kwa ajili ya kumkabidhi Mbunge atakayeshinda zawadi hiyo itakayomuwezesha kusafiri Moja ya nchi atakayochagua Duniani, Kushoto mwenye Jezi ya Simba ni Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Tulia Akson amesema wabunge watatumia Bunge la Bajeti kuandaa Bunge Marathon ambayo itakuwa maalumu kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya wavulana

Dkt, Tulia amebainisha hilo wakati alipokuwa akizungumza na wabunge, watumishi wa Bunge pamoja na watumishi wa taasisi nyingine za serikali na zisizo za kiserikali kwenye uwanja wa jamhuri Jijini Dodoma mara baada ya Wabunge mashabiki na wanachama wa Timu za Simba na Yanga Kumaliza kupapatuana kwenye Michezo mbalimbali.

Amesema mwezi wa nne Mwaka huu kutakuwa na Bunge Marathoni itakayowahusisha wadau pamoja na wananchi wa majimbo mbalimbali kujiunga na kushiriki ili kufanikisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Bunge ya Wavulana itatangazwa baadae kuwa itajengwa wapi, mbayo itakuwa kama ile ya wasichana iliyojengwa Kikombo jijini Dodoma kutokana na fedha walizozipata kutokana na Bunge marthoni ya miaka ya hivi karibuni.

Amesema kila mshiriki atatakiwa kujiunga kwa kuchangia 40,000

“niombe watu wengi wajitokeze kutoka kwenye majimbo ambako wanatoka wabunge, ambapo ukiwa hapa utakimbia na Mbunge wako pamoja na wabunge wengine na hata mimi watu kutoka kwenye jimbo langu wakija nitakimbia nao”, amesema

Kwenye Bonanza hilo lililojumuisha michezo mbali,mbali wabunge na mashabiki wa Yanga wameibuka kuwa washindi wa jumla kutokana na kushinda michezo mbalimbali ukiwemo mpira wa miguu ambayo waliwabugiza wenzao wa simba jumla ya Goli 5.kwa 4 kupitia changamoto ya  mikwaju ya penati baada ya dakika za kawaida kutoshana nguvu kwa kutoka sare ya 1.1

Bunge Spoti Bonanza imedhaminiwa na AZANIA BENK waliyowezesha  maandalizi kabambe ikiwemo kuufunika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma kwa Mango huku Shirika la Ndege La QATAR AIRWAYS likitoa zawadi kwa Mbunge mmoja mshindi Tiketi ya Busness Class kwenda na kurudi nchi yoyote Dunia atakayochagua


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG