Israeli inatengeza propaganda yake ya giza kutokana na uongo na inajaribu kueneza kupitia maafisa, wasomi, na vyombo vya habari, amesema Mkurugenzi wa Mawasiliano Fahrettin Altun.
"Katu hatutakata tamaa kwa kufichua upotoshaji
wa Israeli na kudhihirisha ukweli katika ajenda ya dunia," amesema
mkurugenzi.
Katika hotuba yake kwenye sherehe ya tuzo za TRT
World Citizen Ijumaa, Altun amesema watu wenye fikra za kikoloni wanawatesa
wale wenye fikra tofauti na wao. Amesisita, "Maonevu ya sasa ya Israeli
dhidi ya Palestina, ni kiashiria cha fikra za kikoloni, ambayo inadhihirisha
wazi matendo hayo."
Altun amesema mfumo wa sasa wa kimataifa, ambao
umeanguka katika uso wa udhalilishaji wa Gaza, unaonyesha ni kwa nini kuna
lazima ya kufanyika mabadiliko, na kusema, "Mashirika mengi ya utangazaji
ya nchi za magharibi yanaonyesha kuunga mkono Israeli, kugemea upande mmoja, na
kubadilisha ukweli."
"Katika mashambulizi ambayo yamekuwa
yakiendelea kwa zaidi ya siku 100, Israeli inafanya propaganda za giza na
upotoshaji kupitia vyombo vya habari vya kimataifa na makampuni ya mitandao ya
kijamii."
Kutokana na uwajibikaji wa kibinadamu, Uturuki katu
haibadiliki katika mashambulizi hayo, inasimama pamoja na watu wa Palestina
wanaodhulumiwa, na itaendelea kufanya hivyo, amesema.
Altun amedokeza kwamba, mradi wa tuzo za Citizen
Awards kupitia TRT ni jitihada za kila mmoja kuonyesha uwezo wake wa kuleta
mabadiliko chanya.
'Israeli haitafanikiwa katika
propaganda yake ya giza'
Amesema, mapambano makubwa ya kibinadamu dhidi ya
mauaji ya Israeli yameonyeshwa na waandishi wa habari wanaofanya kazi katika
eneo hilo, Altun amesema kwamba waandishi wa habari "sio tu wametoa
taarifa lakini pia wamepigana katika mapambano matakatifu ya kuonyesha ukweli,
na waandishi 119 wa Palestina wamekufa mashahidi katika jitihada hizo."
Juhudu zisizokuwa za kawaida za waandishi waliopo
Gaza zimepelekea kuwepo kwa wimbi chanya la mabadiliko duniani kote, amesema.
"Sababu kwa nini Israeli imekuwa ikilenga kwa
makusudi waandishi wa habari ni kwa sababu ya ukweli na msimamo wa haki wa
waandishi ...Dunia nzima inajua kwamba Israeli kwa makusudi imelenga waandishi
wa habari kama vile Wael al Dahdouh anaetafuta ukweli, kwa makusudi imeua
familia yake." Ameongeza kwamba, Israeli inajaribu kuuwa ukweli na kuuziba
pumzi."
"Haki pekee yake haitoshi, ni lazima kuwa bora zaidi. Tutapambana katika siasa, diplomasia, msaada wa kibinadamu, mawasiliano, na vyombo vya habari, kumaliza janga hili," ameongeza.
