BANDA MEDIA BLOG

WABUNGE VINARA WAAPA KUUNGANA NA RAIS SAMIA KUPAMBANIA SHERIA YA USAWA WA KIJINSIA

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT), Mary Chatanda akihutubia wakati wa kufunga semina Kikundi cha Wabunge Vinara  Wanawake katika Siasa iliyofanyika jijini Dodoma ambapo walijadili namna ya kwenda kuongeza ushiriki na uwakilishi wa wanawake  katika uongozi na siasa kupitia miswada mitatu inayopelekwa bungeni. Mwenyekiti wa kikundi hicho ni Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Lugangira.

           ......................................................

WABUNGE wanawake wametakiwa kumtua mzigo begani Rais Samia Suluhu Hassani kuhusu uwepo wa sheria sahihi inayojali usawa wa kijinsia katika uongozi mbalimbali.

Msisitizo huo umetolewa na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Chama Mapinduzi CCM, Halima Mamuya na Mary Chatanda wakati wa semina ya Kikundi cha Wabunge Vinara  Wanawake katika Siasa iliyofanyika jijini Dodoma ambapo walijadili namna ya kwenda kuongeza ushiriki na uwakilishi wa wanawake  katika uongozi na siasa kupitia miswada mitatu inayopelekwa bungeni.

 Chatanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT), amesema kuwa wakati wa Mungu wa kuwapigania wanawake ni sasa kwa kumuunga mkono Rais Samia ambaye ni namba moja kwa kupigania suala la usawa wa kijinsia.

Naye Mamuya aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa UWT, amesema kuwa wabunge wanawake na viongozi wengine kupambania usawa wa kijinsia siyo ombi bali ni lazima tuhakikishe tunamtua mzigo begani Rais Samia.



Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG