WHO yaonya magonjwa ya kupumua yameongezeka
Visa vya Uviko 19 vinaendela kuripotiwa sehemu tofauti barani Afrika / Picha: Reuters..........................................................................................
Shirka la Afya Duniani, WHO linaonya kuwa magonjwa ya
mfumo wa upumuaji kutoka Uviko 19, mafua na vimelea vingine vya magonjwa
yamekuwa yakiongezeka katika nchi nyingi kwa wiki kadhaa, na hali hii
inatarajiwa kuendelea.
"Kama watu binafsi hakikisha umepima na kutafuta
huduma inapohitajika kwa sababu matibabu ya Uviko19, yanaweza kuzuia ugonjwa
mbaya na kifo," Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom ameonya.
"Endelea kutumia barakoa, hakikisha hewa safi ya
kutosha mahali ulipo na uhakikishe kuwa wewe na wapendwa wako mmempata chanjo
zinazohitajika za Uviko19.
Wataalamu wa afya wanasema takriban nusu ya waathiriwa wa
Uviko19 katika nchi za Kiafrika wanaripoti angalau dalili moja inayoendelea
ambayo haiwezi kuelezewa na hali zingine za matibabu.
Watafiti wanasema uchovu na dalili zingine zinazoendelea
tayari zinaathiri ubora wa maisha ya watu na zinaweza kudhoofisha uwezo wao wa
kufanya kazi, na kuwafanya wawe katika hatari kupata maambukizi mapya kwa
urahisi.
Ingawa sio tishio la kimataifa tena bado Uviko 19 inaendelea
kuripotiwa katika sehemu tofauti barani Afrika.
Kulingana na Vituo vya kudhibiti Magonjwa Afrika, Africa
CDC tangu janga la Uviko19 kuanza visa 12,216,748 vimeripotiwa barani Afrika
hadi sasa,
Eneo la Kusini mwa Afrika limeripoti visa zaidi.
WHO bado inasaidia serikali kupata uwezo wa kufanya
vipimo vya tishio za afya zizazohusisha kupumua.
" Serikali zinafaa kuhakikisha wananchi wanapata
vipimo vya kuaminika, matibabu na chanjo, haswa kwa wale ambao wako katika
hatari kubwa ya kuambukizwa sana," Adhanom ameongezea.
Mwaka huu Rwanda imeanza kujitayarisha kuzalisha chanjo
aina tofauti mkiwemo chanjo dhidi ya Uviko 19. BioNTech kamouni ya Chanjo
kutoka Ujerumani kimefungua kituo huko Kigali, Rwanda..
Kituo hiki kimeundwa kwa ajili ya kutengeneza chanjo kwa
ajili ya matumizi ndani ya bara la Afrika.
Rwanda sasa itaweza kutoa hadi dozi milioni 50 za bidhaa
kila mwaka .
