Coletta Wanjo
Istanbul, Uturuki
Kiongozi wa Chama cha Upinzani Azimio nchini Kenya,
Raila Odinga ametangaza rasmi nia yake ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Tume
ya Umoja wa Afrika.
"Nimekuwa nikishauriana sana. Nadhani kama niko
tayari kutumikia bara la Afrika. Afrika inastahili ubora zaidi. Niko tayari
kuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika," Raila Odinga amesema katika
mkutano na waandishi wa habari jijini Nairobi nchini Kenya.
Nafasi hiyo kwa sasa ipo chini ya Moussa Faki Mahamat
ambae ni raia wa Chad, ambae aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo.
Awamu yake ya pili ya uongozi inakwisha mwaka huu 2024.
Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo ameuunga
mkono uamuzi huyo wa Raila Odinga, ambae pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Kenya.
"Sina shaka kwamba rafiki yangu huyu ndiye mtu
bora kuchukua jukumu hiyo. Ikiwa kanda ya Afrika Mashariki itamuunga mkono,
basi ataweza," Obasanjo amesema akiwa na Odinga katika mkutano huo wa
waandishi wa habari.
Hii sio mara ya kwanza kwa Kenya kugombea nafasi hiyo
ambayo ni kubwa katika bara la Afrika. Mwaka 2017, Kenya ilijaribu kupata
nasafi hiyo ya juu kupitia mwanasiasa wake Amina Mohammed, aliyekuwa wakati huo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya.
Mwaka 2017 Kenya ilijaribu kupata nasafi hiyo ya juu kupitia mwanasiasa wake Amina Mohammed, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya wakati huo. Picha Reuters
Hata hivyo, Kenya ilishindwa na Chad iliyowakilishwa na Moussa Faki Mahamat.
Raila amewahi kutoa huduma ya kibara.
Aliteuliwa kuwa Mwakilishi Mkuu wa Maendeleo ya
Miundombinu katika Tume ya Umoja wa Afrika mwaka wa 2018. Majukumu hayo
yalikwisha Februari 2023.
Ili kupata kiti hiki, marais wa nchi za Afrika hupiga
kuwa ya siri. Mgombea anahitaji kupata angalau theluthi mbili ya kura, kura 36,
ili
kutangazwa mshindi.
Kazi ya Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa
Afrika ni ipi?
Nchi ambayo inataka kiti hiki hupendekeza nia yake na
kugombea na kumteuwa mtu ambaye atagombea nafasi hiyo.
Ni lazima nchi husika kufanya kampeni katika nchi
tofauti kwani uchaguzi hufanywa na marais na viongozi wa nchi.
Mwenyekiti wa Tume ya AU huchaguliwa na marais wa
Afrika kwa kipindi cha miaka minne. Anaweza kugombea tena kiti hiki mara moja
tena.
Mgombea anahitaji kupata angalau theluthi mbili ya
kura, hiyo ni angalau kura za marais 36, ili
kutangazwa mshindi.
Kazi ya Mwenyekiti wa Tume ya AU
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika ni Afisa Mkuu
Mtendaji, mwakilishi wa kisheria wa AU na Afisa Mkuu wa Uhasibu wa Tume.
Majukumu yake ni pamoja na
- Usimamizi
wa fedha za Tume ya Afrika
- Kuchukua
hatua zinazolenga kukuza na kutangaza malengo ya AU na kuimarisha utendaji
wake
- Kuwezesha
utendakazi, kufanya maamuzi na kuripoti mikutano yote ya mashirika ya AU,
na kuhakikisha ulinganifu na uwiano na sera, mikakati, mipango na miradi
ya AU iliyokubaliwa.
- Kushauriana
na serikali za nchi wanachama wa AU, taasisi nyingine na mashirika ya
kikanda kuhusu shughuli za AU.
- Kuiwakilisha
kidiplomasia muungano wa AU.
- Utayarishaji
wa bajeti wa AU akishirikiana na kamati ya wawakilishi wa nchi za Afrika
katika AU yaani mabalozi.
- Kufanya
kazi kama hifadhi kwa mikataba yote ya AU na OAU na vyombo vya kisheria.
Orodha ya wenyeviti wa zamani wa Tume
hiyo
2017– hadi sasa - Moussa Faki Mahamat, Chad
2012–17- Princess Dlamini Zuma, Afrika Kusini
2008–12 - Jean Ping, Gabon
2003-08 - Alpha Oumar Konaré, Mali
2002–03 (miaka ya mpito ya OAU hadi AU) - Amara Essy, Ivory Coast


