Wanajeshi wawili wa Afrika Kusini wameripotiwa kuuawa na wengine watatu kujeruhiwa baada ya bomu kushambulia kambi yao Picha: SANDF/X
.............................................................................
Wanajeshi wawili wa Afrika Kusini
wameripotiwa kuuawa na wengine watatu kujeruhiwa baada ya bomu kushambulia
kambi yao katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
"Vikosi vya ulinzi vya Kitaifa vya
Afrika Kusini vinathibitisha kwamba mnamo tarehe 14 Februari 2024, mwendo wa
saa saba mchana, bomu lilirushwa ndani ya kambi moja ya kijeshi ya Afrika
Kusini na kusababisha vifo na majeraha," taarifa kutoka Jeshi la Taifa la
Afrika Kusini limesema.
Mapema wiki hii, rais Cyril Ramaphosa
alitangaza kutumwa kwa wanajeshi 2,900 nchini DRC kama sehemu ya kikosi cha
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yenye nia ya kupambana na
makundi yenye silaha. Wanajeshi hao wataendelea kupelekwa nchi DRC hadi Disemba
15, 2024.
"Kutokana na shambulio hilo, maafisa
wawili wa Jeshi la Tafa la Afrika Kusini walikufa na wengine watatu kujeruhiwa.
Walipelekwa hospitali ya karibu ya Goma kwa ajili ya matibabu," taarifa
hiyo imeongezea.
Jeshi la Afrika Kusini limesema bado
hakuna taarifa za kutosha kuhusu mashambulizi haya kwa sasa, wakati uchunguzi
ukiendelea.
Taarifa zaidi kuhusu mauaji ya wanajeshi hao wa DRC zinategemea kuendelea kutoka.
