IKIWA Leo ni siku ya Sita ya Maombolezo ya Hayati Mzee Rukhsa Aliyefariki February 29, na kuzikwa Manga Pwani Zanzibar Machi 2 mwaka huu.
Kumbuka Mzee wa Rukhusa ameandika Changamoto Mbalimbali alizokumbana nazo akiziandika katika kitabu cha Safari ya maisha yake, na hapa anagusia UKIMWI ulivyomletea vikwazo na viongozi wa Dini, endelea Kufuatilia
...........................
Pia kuna Changamoto ya Ukimwi ambapo wakati wa kipindi chake cha kwanza 1985 ndipo ulikuwa umeanza na alikumbana na vikwazo hasa kutoka kwa Viongozi wa dini juu ya matumizi ya kondom. Anadai aliwaambia kuwa yeye anaanzia pale waliposhindwa wao kutowafanya waumini wao wazingatie mafundisho ya dini .
Pia ameongelea siasa za Kikanda ikiwa ni pamoja na juhudi za kuanzisha tena Jumuiya ya Afrika Mashariki na Migogoro ya Rwanda na Burundi na jinsi Tanzania ilivyojitahidi katika utatuzi wake.
Pia mwisho wa Siasa za ubaguzi wa Makaburu wa Afrika Kusini baada ya Mandela kuwa Rais na namna Mwenge wa Uhuru uliokuwa umebeba dhana ya Ukombozi wa Afrika na mbio za mwenge kuonekana ni suala la CCM na namna walivyobadilisha kuwa za kitaifa kwa ajili ya kuzindua miradi ya maendeleo
Mzee Rukhsa hajaandika vya kutosha kuhusu familia yake zaidi ya picha tu. Lakini amejitahidi kuelezea namna alivyokabiliana na changamoto za uongozi wake
Kwa hakika naweza kusema alikuwa Rais Mwana Demokrasia, Aliyechagiza Mabadiliko kwa Vitendo.
Siku za Maombolezo mwisho Machi 7,2024 ambapo Hitma ya mwisho Itasomwa..!!!
