BANDA MEDIA BLOG

JUHUDI ZETU WANAWAKE HAZIPOTEI BURE- CDE. MWAJABU

WANAWAKE wa wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es lam wamehimizwa kuendelea kuelimisha jamii juu ya usawa wa kijinsia na kupinga ukatili haswa kwa watoto.

Witi huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) Mkoa wa Dar es salaam Mwajabu Mbwambo, kwenye  hafla ya Usiku wa Mwanamke wa Kigamboni akiwa ndiye Mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika Katika Ukumbi wa Barakuda uliyopo Mji Mwema.

Katika hotuba yake, Bi. Mwajabu ametanguliza shukrani kwa uongozi wa Halmashauri ya manispaa ya Kigamboni kwa kumteua kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo kwani ni heshima kubwa kwake.

Bi. Mwajabu ametoa wito kwa Wanawake wote kuwa na moyo wa kushikana mikono, kuinuana na kupeana fulsa mbalimbali katika kupelekea kuinuka kwenye uchumi wa kati.

"Nitoe pongezi kwetu sote wanawake kwani juhudi zote tunazofanya wanawake hazipotei bure kwakuwa kwa pamoja tunainuana na ndio dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,

"Kupitia Serikali, Taaisisi na Mashirika binafsi, Wanawake tumekuwa tukiwezeshwa katika kuingia kwenye uchumi wa kati na kupelekea kuwa chachu ya maendeleo kuanzia kwenye familia hadi jamii kwa ujumla na hali hii imeakisi moja kwa moja kwenye kauli mbiu yetu,

"Wanawake tuendelee kuelimisha jamii juu ya usawa wa kijinsia na kupinga ukatili haswa kwa watoto na hii ianzie majumbani kwetu katika kutoa Elimu kwa watoto namna ya kuweza kujiepusha na majanga haya."

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG