BANDA MEDIA BLOG

DC BULEMBO ATAKA WANAWAKE WA KIGAMBONI KUENDELEA KUSHIKAMANA


"Niwashukuru wanawake wa kigamboni  wakati wote mmekuwa baraka kwangu kila jambo mmekuwa mkinisapoti, hakuna sehemu ambayo mmeniangusha nami naendelea kuwaomba ushirikiano na kushikana mikono"

"Asanteni kwa kuona kazi nzuri ninayofanya ila niwape siri kazi hii ni kwa kushirikiana na Katibu tawala wetu Dada Pendo Mahalu hakika amekuwa msaada mkubwa kwangu naye Afisa Maendeleo Jamii Wilaya Bi. Sigilinda Mdemu hakika anachapa kazi yupo shapu sana na amekuwa sehemu ya kiunganishi kwa Wanawake wa Kigamboni."

"Tarehe 8 siku ya Ijumaa mwezi huu ndio kilele cha Siku ya Wanawake Duniani na kimkoa tutaadhimisha ndani ya Wilaya yetu ya Kigamboni na Mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa Mhe. Albert Chalamila hivyo niwaombe tujitokeze kwa wingi kushiriki"

"Vilevile niwaombe Wanawake wote Kigamboni tujitokeze kwa pamoja kuna jambo pale Diamond Jubilee ambapo Mgeni rasmi atakuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mama yetu tunampenda na tuendelee kumuunga mkono"

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo wakati alipokuwa Kizungimza na wanawake wa wilaya hiyo usiku wa kuamkia Leo Kwenye Usiku wa Wanawake wa Kigamboni.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG