.........................................................................................
WAZIRI wa mipango wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Judith Sumimwa Tuluka Jumatatu amekuwa Wari mkuu wa Kwanza Mwanamke katika Taifa hilo la Africa ya Kati, Televisheni ya Serikali Imetangaza
Waziri huyo mkuu mpya, ni
mchumi na amechukuwa nafasi ya Jean Michel Lukonde kufuatia ushindi wa kishindo
wa muhula wa pili wa Rais Felix Tshisekedi kwenye uchaguzi wa tarehe 20 Disemba
mwaka jana.
Tuluka alisema kupitia televisheni ya taifa kwamba “kazi ni kubwa, changamoto
ni kubwa lakini kwa pamoja tutafika”.
“ Ninafahamu jukumu kubwa
linalonisubiri,” aliongeza, akisema anataka kufanya kazi “kwa ajili ya amani na
maendeleo” ili “wananchi wa Congo wanufaike na rasilimali” za nchi.
Tshisekedi alishinda rasmi
kwa asilimia 73.47 kwenye uchaguzi wa Disemba ambao ulifanyika kwa amani kwa
kiasi kikubwa katika nchi inayokumbwa na ghasia na ukosefu wa usalama.
Lakini upinzani ulidai
uchaguzi uligubikwa na udanganyifu.
Waziri mkuu mpya atakuwa na
jukumu la kutekeleza vipaumbele vilivyotangazwa na rais kuhusu ajira, vijana,
wanawake na uwiano wa kitaifa katika taifa hilo la takriban watu milioni 100.
Tshisekedi alikuwa rais mwaka
2019 akiahidi kuboresha maisha nchini DRC, nchi yenye utajiri wa madini lakini
yenye raia wengi maskini, na kumaliza umwagaji damu wa miaka 25 mashariki mwa
nchi.
