..................................................................
NA JOHN BANDA, DODOMA
APRILI 1, 2024 Kumefanyika
ibada ya kuliombea Taifa la Tanzana iliyofayika katika Uwanja wa Jamhuri jijini
Dodoma ikiandaliwa na Umoja wa Madhehebu ya Kikisto huku Mgeni Rasmi akiwa mkuu
wa Mkoa huo aliyewakirishwa na Mkuu wa Wilya wa Chamwino Janeth Mayanja.
Akiwasilisha Salamu za Mkuu
wa Mkoa Mayanja ameipongeza kamati hiyo ya maandalizi kwa kutoa ushirikiano wa
hali na Mali kwa serikali hali inayosababisha shughuli za Mkoa kwenyika kwa
urahisi.
Aidha ameupongeza umoja huo
kwa kuwa na Ubunifu wa Kuombea Nchi na Familia kwa lengo la kuhakikisha haki,
Amani na Upendo vinadumu hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.
Mayanja amewakumbusha
Viongozi wa Dini kuhakikisha wanaendeleza vipindi vya Watoto makanisani kwa
Lengo la kuendelea kufundisha vijana na Watoto umimu wa kulinda na kuyadumisha
Maadili mema.
“wakati ninyi mnaikumbusha
serikali kuhusu kusimamia maadili ili kuwakinga watoto wetu na Mmomonyoko wa
Maadili unaotokana na utandawazi uliyopo katika jamii ya watanzania, na mimi
niwaombe kuendeleza vipindi vya vijana na Watoto katika makanisa vitavyowajenga
Watoto katika maadili mema,
Tuwekeze nguvu kubwa katika
kuwajenga Watoto na vijana wetu, katika maadili bora badala ya kuhangaika na
watu wazima kwani Samaki mkunje angali mbichi, tukawambie kuhusu ubaya wa
vitendo vya Ushoga, usagaji, ubakaji, matumizi ya vilevi, madawa ya kulevya,
chuki, visasi na migogoro isiyona tija, badala yake wakawe watu wema katika
jamii na kwa njia hiyo tutakuwa tumelijenga taifa Bora la Watanzania”, amesema
Pamoja na kuwapa Watoto elimu
ya Dunia lakini pia tuhakikishe tunawafundisha elimu ya Dini, hasa siku za mwisho
wa wiki ambazo Watoto wanakuwa mapuziko wasiishie kuangalia katuni kwenye Tv au
magemu kwenye simu badala yake jamii iwafunze Watoto elimu ya Dini.
Katika hatua Nyingine DC huyo
amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu hassani kwa kuwatengenezea watendaji wa
serikali mazingira mazuri katika maeneo yao ya kazi kwa kutekeleza Miradi
mbalimbali ya kimaendeleo, tofauti na vipindi vya Nyuma ambavyo walikuwa wanapata
kigugumizi hata kufanya ziara vijijini kwa kuhofia kuulizwa maswali yasiyo na
majibu.
“rais Samia ametufanya
watetendaji wa serikali na wateule wake tuwe na ujasiri wa kufanya ziara kila
mahali bila kuhofia kuulizwa maswali na wananchi yasiyo na majibu, kwani kila
unapokanyaga unakuta Mradi uwe wa Elimu, maji, afya, Umeme au miundombinu ya
Barabara unatekelezwa hakika ameweka historia kubwa katika uongozi wake kwa
kutatua kero za wananchi”, amesema Mayanja
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Madhehebu ya Kikristo yayounganisha TEC, CPCT na CCT, Anthon Mjashimba ambaye
pia ni Askofu wa Kanisa la Babtist kanda ya kati, amesema katika Mkoa wa Dodoma
hakuna Shari wala Swali katika umoja huo.
“umoja wa madhehebu ya
kikristo mkoani kwetu hakuna ile nani bora au nani siyo bora katika ibada zetu,
sisi sote ni kitu kimoja tumepatana kufanya kwa Pamoja, ndiyo maana tunakutana
kufanya maombezi kwa ajili ya taifa, serikali, viongozi na jamii kwa ujumla pia
tunafanya makongamano mbalimbali na hata mwezi wa saba mwaka huu tunakutanisha
kwaya zetu Zaidi ya 100 kwenye tamasha moja”. Amesema
Amesema lengo la Ibada ya
Pasaka pili ni Kukumbuka kifo na kufufuka kwa Yesu Mkombozi wa Ulimwengu, Lengo
la Pili likiwa ni kuliombea Taifa ili haki ikatendeke kwenye Uchaguzi ujao wa
Serikali za Mitaa na ule Mkuu wa Mwaka Ujao ili taifa livuke salama.
Nae Katibu wa Umoja wa Wanawake
wa CCT, Tanzania ambeye ni mratibu wa Shughuli za Wanawake na Watoto, Magreth Masawa amewashauri wanawake ambao wana jukumu
kubwa la malezi ya familia kuhakikisha wanawafundisha kwa kuwasemesha Watoto wao
tangu siku ya kwanza ya kutunga mimba Pamoja na kuwaombea waweze kuwa katika
maadili mema yenye kumpendeza Mung una jamii kwa ujumala.