BANDA MEDIA BLOG

MASHINDANO YA QUR’AN YA VYUO VIKUU NA VYA KATI YAFANYIKA DODOMA.


Prof. Fadhil Mgumia akimkabidhi zawadi ya ushindi wa kusoma Qur'an kwa ufasaha Mwanafunzi kutoka  Chuo cha Saint John Hassan Suleimani aliyeibuka Mshindi na kuzawadiwa cheti na Fedha Taslimu.        

 ………………………………………………………

NA JOHN BANDA, DODOMA

MASHINDANO ya Qur’ an kwa wanafunzi wa Vyuo vikuu na vya kati Mkoani Dodoma yamefanyika Aprili 6,2024 ikiwa zimesalia siku chache kukamilika kwa Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani huku msisitizo ukiwa ni kwa waumini wa Dini ya Kiislamu kuendea kuyaishi mafunzo waliyoyapata.

Akizungumza baada ya mashindano hayo Mlezi wa Wanafunzi wa Kiislamu wa Chuo cha Mipango, Prof. Fadhil Mgumia amesema  mwezi wa Ramadhin Umejaa Kheri nyingi, Rehema Nyingi ni mwezi Mtukufu na ni mwezi wa Mfunzo ambapo Waumini hufanya Ibada Nyingi wakitoa na Sadaka.

“mwezi huu ni kama chuo tunafundishwa namna ya kuishi kama waislamu, basi hata mwezi unapoisha tuendelee kuwa waislamu tunaosali, kutoa sadaka, kusoma QUR’AN na kuendelea kushindana katika kuisoma,

Kama mwezi Mtukufu wa Ramadhan ni Chuo nategemea mwezi utakapoisha tutaendelea na yale tuliyofundishwa ndani ya mwezi huu”, amesema

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Fahmi Ali Hassan amesema jumla ya wanafunzi 31 kutoka vyuo vya UDOM, Serikali za Mitaa Hombolo, St. John na Mipango yenyewe ndiyo walioshiriki huku mwanafunzi kutoka Chuo cha Saint John Hassan Suleimani akiibuka Mshindi na kuzawadiwa Fedha Taslimu.



Mmoja wa waalikwa kwenye mashindano hayo mkurugenzi wa Wema Takaful Agency Ltd, wakala wa kampuni inayotoa huduma za kibima kwa kuzingatia Shariah ya Kiislam ndugu Ally Ally amewataka Waislamu na Watanzania kwa ujumla kujiunga na Bima hiyo

Amesema Bima hiyo inakidhi viwango kwa kuzingatia makatazo yote ya kisheria kwani haina Riba wala kupoteza kama kucheza kamali isiyo na udanganyifu.

ukikata Bima hii unashiriki katika mfumo wa uchumi unaoafikina na Sheria za nchi, mteja hawezi kupoteza kama aliyecheza kamali, inatoa gawio kila mwaka kwa mteja ambaye hajadai, inakuza maadili na uwajibikaji kwa jamii lakini pia anashiriki katika uwajibikaji wa Pamoja na kupata gawio la faida”, amesema 














Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG