BANDA MEDIA BLOG

WATUHUMIWA MBARONI KWA KUTAKA KUTOROSHA MIFUGO NJE YA NCHI

 

1000708759

Na. Abel Paul, Jeshi la Polisi- Namanga Arusha.

Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wakitorosha mifugo 514 Kwenda Nchi Jirani huku wakitumia vibali vya kampuni isiyohusika na Mifugo hiyo.

Akitoa taarifa hiyo kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo Nchini kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua amesema Kikosi hicho kwa kushirikina na wananchi Aprili 06,2024 Katika Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha waliwakama watu wawili wakiwa na mifugo 514 ambayo walikuwa wakiitorosha Kwenda nchi Jirani.

Kamanda Pasua amebainsha kuwa watuhumiwa hao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi huku akiwaomba wananchi kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na utoroshaji na kukiuka taratibu za uuzaji wa Mifugo hapa Nchini.

SACP Pasua amesisitiza na kuwataka wananchi kufuata taratibu za uuzaji wa mifugo ili kutokukumbana na mkono wa sheria na kulikosesha mapato Taifa huku akisema Jeshi hilo litaendelea kuwakamata wale wote watakao kiuka taratibu.

Nao baadhi ya wafanya biashara wa mnada huo wa mpakani Namanga wamewaomba wananchi wenzao kufuata taratibu zilizopo ili kutokukumbana na mkono wa sheria pindi wanapotaka kusafirisha mifugo yao nje ya nchi.

Daktari wa Mifugo Mnada wa Mpakani Namanga Longido Mkoani Arusha amewataka wafanya biashara kufuata taratibu huku akiwaomba wafanya biashara hao kufika na vibali vilivyo kamilika ili kuondoa usumbufu na wasimamizi wa Mnada huo.
1000708757
1000708753
1000708758
1000708754
1000708756
1000708755

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG