OR - TAMISEMI
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainabu Katimba
ameahidi kuendeleza ushirikiano na watendaji wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI ili
kutimiza azma ya Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kutoa huduma bora kwa
wananchi.
Mhe. Katimba ametoa ahadi hiyo leo Aprili 5, 2024
Jijini Dodoma mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI
yaliyopo katika Mji wa Serikali Mtumba.
Mhe. Katimba ameahidi kuendelea kushirikiana
kiutendaji na watumishi wote ili kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI
kwa uadilifu na weledi.
“Ninawaomba tushirikiane, nami ninaahidi kuwapa
ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya ofisi kwa lengo la kutoa huduma bora
kwa wananchi” amesisitiza Mhe. Katimba
Naye, Naibu Waziri Ofisi ya RAIS –TAMISEMI
anayeshughulikia Afya Dkt. Festo Dugange amewataka watumishi wa Ofisi ya Rais
TAMISEMI kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Mhe. Katimba ili aweze kutekeleza
majukumu yake ipasavyo.
Mhe. Zainabu Katimba aliapishwa tarehe 04 Aprili 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI.


