Mratibu wa Dawati la Maendeleo ya Wanawake, Jinsia na Watoto CCT, Shemasi Ester Mahagachi akielekeza jambo wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya Uongozi, Uundwaji wa Vikundi na Usimamizi wake yaliyofanyika jijini Dodoma
Rey Conon Dkt. Margareth Ndonde ambaye pia ni Katibu wa Wanawake wa Kanisa la Anglikana Tanzania akiimba pamoja na washiriki wa mafunzo hayo wimbo wa Tanzania Nakupenda uliomo katika Albamu yake yenye nyombo 8 ikienda kwa jina la Mungu wetu ni wa Ajabu
..........................
NA JOHN BANDA, DODOMA
MRATIBU wa Dawati la Maendeleo ya Wanawake, Jinsia na
Watoto CCT, Shemasi Ester Mahagachi amewaasa
waratibu na makatibu wa Ushirika wa mama wa kikristo Tanzania (UMAKI) Kugombea
nafasi za Uongozi kwenye Uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa na zile za
Udiwani na Ubunge utakaofanyika mwaka ujao.
Bi. Ester ameutoa Wito huo wakati alipokuwa akifunga
mafunzo ya Uongozi, Uundwaji na Usimamizi wa Vikundi vya akiba na mikopo kwa Waratibu
wa Kanda na Makatibu wa Umaki toka Dayosisi 16 za kanisa Anglikana Tanzania
waliokutana kunoana jijini Dodoma.
“wengi wetu tumepitia mafunzo mbalimbali na tuna
zoefu katika uongozi Tunapoenda kwenye maeneo yetu kuongoza tusiishie tu
kanisani twendeni tukachukue fomu za kugombe uongozi wa kijamii, si tunajua
kuwa mwaka huu ni uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo pia ni maandalizi
kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani?” amesema na kuhoji,
Tuna nguvu na tuna uwezo wa kuongoza tukajitokeze, kugombea kwani siyo dhambi, kumbuka usipojitokeza wewe kugombea watajitokeza wengine na watakuongoza baada ya
kuchaguliwa”, amesema
Aidha amesema “Nenda karekebeshe kumbukumbu zako
kwenye daftari la mpiga kura lakini wakati ule wa uchaguzi nenda kapige kura
maana usipoenda wewe wengine watamchagua mtu ambaye hukumuhitaji hata kama hana uwezo na atakuongoza
utake usitake”,
Awali Mratibu wa Kanda ya Magaribi, Judith Kaigarula wakati akisoma Risala mbele ya Mgeni Rasmi,
mafunzo hayo yaliwashirikisha Waratibu wa kanda 4 za Kaskazini Mashariki, Kanda
ya Ziwa, Kanda ya Kati na kanda ya Magaribi Pamoja na Makatibu wa Umaki wa
Dayosisi 16 kati ya 28 za Bara na Visiwani.
Ambapo amesema mafunzo mengine waliyoyapata ni Pamoja
na kuzitambua rasilimali zilizowazunguka makanisani na kisha kuzitumia kwa
ajili ya maendeleo ya kanisa na watu wake.