Wanajeshi wa DRC wamekuwa wakiendesha vita kwa miongo kadhaa iliyopita dhidi ya makundi ya wapiganaji walioko mashariki mwa nchi hiyo. /Picha: Reuters
Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la
"Allied Democratic Forces" (ADF), wanaoaminika kuwa na uhusiano na kundi
la Daesh, wamewaua takriban watu 10 katika shambulio la usiku katika kijiji
kimoja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, afisa wa eneo hilo na
kiongozi wa mashirika ya kiraia alisema Jumamosi.
Watu wenye silaha walishambulia kijiji cha Masala
katika eneo la Beni, kilicho katika mkoa wa Kivu Kaskazini, usiku wa kuamkia
leo, msimamizi wa kijeshi Charles Euta Omeonga aliambia Reuters kwa njia ya
simu.
Kiongozi wa mashirika ya kiraia Justin Kavalami
alisema shambulio hilo lilitekelezwa na wanachama wa ADF, kundi lile lile
ambalo afisa wa eneo hilo alilishutumu kwa kuhusika na shambulio lingine la
kijiji ambalo liliua takriban watu 16 mapema wiki hii.
Kavalami alisema zaidi ya watu 13 waliuawa katika
shambulio la Masala.
ADF wanatokea nchi jirani ya Uganda. Sasa ikiwa na
makao yake mashariki mwa Kongo, imeahidi utiifu wake kwa kundi la Daesh na
kufanya mashambulizi ya mara kwa mara, na kuzidi kuyumbisha eneo ambalo makundi
mengi ya wanamgambo yanaendesha harakati zao.
Reuters ilisema haikuwezekana kupatiana kwa maoni ya
ADF.
