BANDA MEDIA BLOG

DKT. JAFO APONGEZA UWEKEZAJI KIWANDA CHA SUKARI KILOMBERO




Na Mwandishi Wetu, MOROGORO 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo leo  ameupongeza uongozi wa kiwanda cha sukari Kilombero  kilichopo mkoani Morogoro kwa uwekezaji mkubwa na kwasasa kinafanyiwa upanuzi mkubwa wa gharama ya sh. Bilioni 650.

Uwekezaji huo utaongeza uwezo wa uzalishaji wa sukari kutoka Tani 130,000 za sasa hadi Tani 270,000  na hivyo kuchangia kuondoa upungufu wa sukari hapa nchini.

Akizungumza Julai 31, 2024 alipotembelea kiwanda hicho, Waziri Jafo amekipongeza pia kiwanda hicho kwa kuchangia upatikani wa ajira hapa nchini.

 "kwasasa kiwanda hicho kimeajiri wafanyakazi 4500 huku  wakulima 11,000 wamewezeshwa na wanauza miwa yao kiwandani hapo na  mapato yanayokwenda kwa wakulima hao ni wastani wa sh. bilioni 67 kwa mwaka."amesema Dkt.Jafo

Dkt. Jafo amewahakikisha wawekezaji wote hapa nchini kwamba serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan  inawapongeza wawekezaji wote na itaendelea kulinda uwekezaji wa viwanda vya aina mbalimbali vilivyopo  hapa nchini kwa lengo kukuza uchumi na kulinda ajira za watanzania.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG