Askofu wa Dayosisi ya Rifty Valley mkoani Singida, John Lupaa akikabidhi msaada wa Godoro, Branket na Mahindi kilo 60, kwa mmoja wa wahanga wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizoambatana na upepo mkali, yaliyotokea mwezi januari mwaka huu katika kijiji cha sasajila wilayani Manyoni.
Katibu wa Umoja wa wanawake wa Kikristo Tanzania (UMAKI) Dkt, Ley Canon Margareth Ndonde, akitoa msaada huo kwa mmoja wa waathilika
Mke wa Askofu Devota Lupaa akitoa msaada kwa mmoaja wa waathilika hao
(PICHA ZOTE NA JOHN BANDA)
Katibu wa Umoja wa wanawake wa Kikristo Tanzania (UMAKI) Dkt, Ley Canon Margareth Ndonde, akizungumza jambo kwenye Ugawaji wa Misaada hiyo.
(PICHA ZOTE NA JOHN BANDA)
............
NA JOHN BANDA, SINGIDA
KANISA Anglikana Tanzania, limetoa msaada wa Vyakula,
Magodoro na Mabranketi yenye thamani ya Zaidi ya milioni 18 za Kitanzania kwa kaya
Zaidi ya 100 zilizokumbwa na mafuriko januari kwaka huu katika Kijiji cha Sasajila
kata ya chikuyu wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Akiongea Julai 22,2024 nje ya kanisa la Mtakatifu
Methew Anglikana Sasajila, mara baada ya kukabidhi Misaada hiyo Askofu wa Dayosisi
ya Rifty Valley mkoani Singida, John Lupaa amesema kanisa anglikana Tanzania
kwa Kushirikiana na Dayosisi hiyo wametoa msaada huo kwa wahanga waliokumbwa na
mvua zilizoambatana na Upepo mkali.
Amesema Mvua hizo zilisababisha uhalibifu mkubwa wa
mali za wakazi Zaidi 165, wanaotoka kaya 104 katika Kijiji cha Sasajila, kata
ya Chikuyu wilayani humo ambapo Nyumba za makazi, Vyakula na mali nyingine vilihalibiwa
na kuwafanya wakazi kukosa makazi.
“kigezo kilichotumika kuwapa misaada hii ni kutokana
na watu hawa kukosa makazi na vyakula kutokana na nyumba, mazao waliyokuwa
wamelima kusombwa na maji wakati wa mvua
hizo za mwezi januari mwaka huu”, amesema
Kwa Upande wake Katibu wa Umoja wa wanawake wa Kikristo
Tanzania (UMAKI) Dkt, Ley Canon Margareth Ndonde amesema moja ya kazi za kanisa
ni kuwafikia watu wenye uhitaji, wakiwemo walikuombwa na Madhila mbalimbali kama
hayo yaliyosababishwa Mvua za Upepo mkali.
“kanisa limetoa msaada wenye thamani ya sh. Milioni 18 tukijua msaada huo utawasogeza sehemu, maana wao hawakujitakia bali ni kutokana na majanga ya asili na kwamba wataendelea kuwaombea”, amesema Dkt. Ndonde aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa kanisa Anglikana Tanzania, Mchungaji/ Canon Bethael Mlula
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Weza B. Bonface Mahajile
amesema msaada huo utatumika vizuri, kwa kuwa atahakikisha anawafuatilia
wahanga 48, wanaotoka katika kitongoji chake ili kuhakikisha hakuna anayeuza au
kutumia vibaya msaada huo uliotolewa na kanisa la Anglikana.
Nae Chapa Muganda mwenye asili ya kisukuma, akiongea kwa Kiswahili cha
kubahatisha kutokana na kutokijua sawasawa na Anjelina Msangu wamelishukuru
kanisa la Anglikana kwa kuwapa msaada huo ambapo chakula hicho kitawasogeza kwa
Zaidi ya miazi miwili.
Mvua zilizoambatana na upepo zilisababisha mafuriko katika Mikoa ya Tanzania Kuanzia januari mwaka huu, Mpaka katikati ya Mwezi wa Nne ambapo yalisababisha maafa makubwa, yakiwemo ya watu kupoteza Maisha, Mali, vyakula na nyumba za makazi.