BANDA MEDIA BLOG

KASISI WA MIAKA YA 1968, ASEMA DCT ITAKUWA TISHIO, CHILONGANI ALIGOMEA KANISA MASIKINI….

Askofu wa kanisa Anglikana DCT, Dkt. Dickson Chilongani akifurahia jambo kwa kushikana Mkono na Mchungaji Canon Mstaahu Hosea Chibago, walipokutana katika kanisa la Mtakatifu Petro Kisasa ambapo Askofu huyo amewawekea mkono wa Kipaimara wakristo 84. 



Sehemu ya wa wanafunzi waliopandishwa daraja la Ukristo kwa kuwekewa kipaimara na Askofu wa DCT, Dkt. Dickson Chilongani,

(PICHA ZOTE  NA JOHN BANDA)

…………….

NA JOHN BANDA, DODOMA

KANONI Mstaafu, Hosea Chibago ambaye kwa sasa ametimiza umri wa miaka 89 tangu kuzaliwa kwake, na ambaye amepata kuhudumu ndani ya kanisa la Anglikana Tanzania,  Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) katika nafasi mbalimbali za uongozi tangu mwaka 1968 amesema miaka michache ijayo kanisa hilo litakuwa tishio kiuchumi na kimaendelo hapa nchini.

Chibago ambaye mwaka 1968, alikuwa na cheo cha kateksiti anasema hivi sasa kutokana na Ukomavu wa Wakrito wa DCT, walioanza kujengwa tangu miaka ya nyuma Ambapo kanisa lilikuwa na mradi wa kutoa  elimu ya kuwafunza kusoma na kuandika uliojulikana kwa jina la TIMU, walipofaulu walipewa Biblia na kisha baadae kuwabatiza.

“wakati ule hasa huko vijijini watu wengi walikuwa hawajui kusoma na kuandika hivyo kanisa likaja na mradi wa kuwasomesha ulioitwa TIMU na walipojua kusoma na kuandika walipewa biblia na kuukubali ukristo wa anglikana’, amesema

Mstaafu huyo ambaye mwaka 1977, aliwekewa mikono na kuwa mchungaji Rasmi na baadae kuwa CANON cheo ambacho kilimsogeza katika ofisi ya Askofu wa DCT na kuwa mshauri wake mpaka alipostaafu mwaka 2004, anasema kanisa limekuwa na miradi mbalimbali ikiwemo ya ufugaji wa kuku, mbuzi, ng’ombe wa maziwa, lakini pia utoaji wa Elimu na Afya kwa jamii kwa lengo la kujijenga kiuchumi na kujiletea maendeleo.

Amesema kwa sasa kanisa linaelekea kwenye maendeleo makubwa ya kiuchumi kwani hivi sasa baada ya DCT, kukamilisha na Kuzindua jengo la Kitega uchumi la SAFINA lililopo kanisa kuu la Roho mtakatifa mwaka 2023, Askofu aliyopo madarakani Dkt. Dicksoni Chilongani amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha ujengaji wa vitega uchumi katika maeneo ya mapareshi.

“ninachokiona miaka michache ijayo DCT hatashikika kiuchumi na kimaenendeleo itatisha katika Madayosisi yote hapa Nchini”, amesema

Ameongeza kuwa Wachangaji ili waweze kufanya kazi ya Mungu vizuri, katika kulichunga kanisa hutegemea sadaka ili waweze kujikimu katika Maisha, lakini sadaka zimekuwa hazitoshelezi na pia huwezi kuwakamua washirika Zaidi ya uwezo wao lakini kwa kuanzisha miradi itasaidia makanisa kuwa na nguvu za kuhudumia watumishi vizauri, huku kazi ikisonga mbele kwa furaha na amani.

ASKOFU DKT. CHILONGANI

Kwenye Kanisa la Saint Peter Parishi ya Kisasa likiungana na Msamalia Mwema la Ilazo jijini Dodoma, julai 14,2024 Askofu Dicksoni Chilongani amewawekea Mikono na kuwaingiza katika daraja la Ukrito, wakristo 84, wanaume na wanawake, ambapo baada ya huduma hiyo anayataka makundi ya kwaya kuanza kujitafutia maeneo ya kuwekeza ili kuepuka kuomba michango kila wakati.

“kama ambavyo Parishi zimeanza kuwa na kasi ya kuweka vitega uchumi katika maeneo ya makanisa yao kwa kujenga fremu za Biashara, vyoo vya kisasa vya kulipia, naagiza hata makundi ya kwaya kuanza kutafuta maeneo ya kuwekeza miradi yao ambayo itawasaidia kupata fedha za kujiendesha badala ya kutegemea kuomba michango kila inapotokea safari za kihuduma’, amesema Dkt. Chilongani

Aidha Akofu huyo amesema anataka kanisa linalokuwa kiroho na Kiuchumi.

“mwaka 2022 tulibatiza wakristo Elfu 13,  mwaka 2023 tulibatiza elfu 18 leo nimewawekea mikono 89 jana 300 bado naendelea na huduma hiyo haya yote yanatokana na kujitoa kwetu kufanya uinjilisti,

Uinjilisti uende Pamoja na uwekezaji, kama ninavyosema mara nyingi sitaki kanisa masikini, kanisa masikini haliwezi kutimiza utume wake, tunataka kanisa linaloweza kutimiza utume kwa vyanzo vyake vya ndani”, amesema na kuongeza

DCT. Ina jumala ya Parishi 300 zenye wachungaji 300 huku kukiwa na makanisa madagomadogo 1264, mwaka uliopita jumla ya walioingizwa kwenye daraja la Ukristo, kwa kuwekewa kipaimara walikuwa 992 ambayo ni kasi kubwa ya ukuaji wa kanisa hilo ambalo lina mpango miaka ijayo kwenda Ulaya ambako  kwa sasa kanisa linalegalega kwa ajili ya kupeleka injili kwa kujigaramia lenyewe.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG