BANDA MEDIA BLOG

ACHIMWENE SAFARI, WAISHURU LATRA KWA KUTAMBUA MCHANGO WAO KATIKA USAFIRISHAJI ABALIA

  

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Daniel Sillo akiwa pamoja na maofisa wa mabasi ya kampuni ya Achimwene Safari katika picha ya pamoja mara baada ya kuwakabidhi chiti na tuzo ya ushindi.

                                 ..............

                     NA JOHN BANDA, DODOMA

KAMPUNI ya ACHIMWENE SAFARI, inayotoa huduma za Usalishaji abaria kwa kwa kutumia Mabasi, wameipongeza Mamlaka ya Usafirishaji Ardhini (LATRA) kwa kutambua mchango wao katika sekta ya usafirishaji.

Wakizungumza na  hili kwa nyakati tofauti wamesema LATRA imetoa vyeti vya pongezi na Tuzo kwa kutambua kazi nzuri wanayofanya.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Achimwene Safari, Henerico Yohana  ameishukuru LATRA kwa kutambua mchango wao kwa kutoa huduma nzuri ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usalama wa abilia na mali zao.

Yohana amewasisitiza madereva wake kuhakikisha wanazingatia sheria za barabarani ili kudhibiti ajali zinazo sababishwa na makosa ya kibinadamu ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya watu.

“Tunaishukuru sana LATRA kwa hizi tuzo ambazo zimetolewa leo zinaendelea kutupa hamasa katika shughuli za usafirishaji. Natoa wito kwa madereva wangu kuwa makini barabarani na kuwahudumia watu vizuri huku wakijali usalama wa abilia,”alisema

Aliongeza kuwa:”Mikakati waliyonayo ni kuhakikisha wanaendelea kuchukua tuzo na kusafirisha abilia na mali zao huku suala la usalama likiwa ni kipaumbele chao,”

kwa Uande wake Mtendaji mkuu wa Kampuni hiyo Innocent Joseph amesema kutokana na huduma zao kupokelewa vizuri wataendelea kutanua wigo wa huduma zao za usafiri ili kuifikia mikoa ambayo bado mabasi hayo hayajaanza kufika.

"usalama ni wa kutosha achimweno safari ni rafiki wa safari", ameongeza Joseph 

Kwa mujibu wa LATRA ilitoa tuzo kwa wasafirishaji wenye mabasi kati ya matatu hadi 10  ambapo mshindi wa kwanza alikuwa ni Sama Luxuary, mshindi wa Pili ni Achimwene Safari na watatu akiwa ni Satco.

Tuzo hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Daniel Sillo kwa niaba ya Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango.


1 Comments

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG