BANDA MEDIA BLOG

CHUO CHA BENKI KUU CHASISITIZA MAADILI KWA WANAFUNZI

 Chuo cha Benki Mwanza kimemeendela kuwajenga wanafunzi kwenye maadili ili kuhakikisha wanawapata watendaji wazuri watakaosimamia suala la maadili katika sekta ya fedha.

Hayo yamebainishwa Leo Agosti 3, 2024 na  Asumpta Muna Wakati akizungumza na Fullshangwe Blog katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea kufanyika Nzuguni Jijini Dodoma.

Amesema chuo hicho kinamajukumu ya kutoa elimu kwa umma kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi sanjari na sula la maadili.

Ameeleza kuwa mafunzo ya muda mfupi ni kuwajengea uwezo wafanyakazi walioko kwenye sekta ya fedha ili waendelee kuongeza weledi na ujuzi utakao leta tija katika kazi zao.

“Kutokana na mafunzo haya kuwa mahili pia yamevutia nchi jirani ikiwemo Kenya, Uganda, Burundi, Msumbiji,Ghana, Malawi, Zambia hizi ni baadhi ya nchi ambazo zimekuwa zikileta washiriki kutoka katika benki kuu za nchi hizo kuja kufanya mafunzo katika Chuo chetu kwa lengo la kuendelea kuwajengea uwezo wafanyakazi wao”, amesema

Amesema Chuo hicho kinatoa mafunzo ya muda mrefu katika kozi mbili ikiwemo astashaada ambayo ni kozi ya miaka miwili na tunachukua wanafunzi ambao wamemaliza kidato cha sita ambao wana malengo ya kufanya kazi katika sekta ya fedha.

Aidha, amesema kuwa Chuo hicho kimefungua dirisha la udahili ambao unaendelea hadi mwezi wa tisa hivyo wanawakaribisha watu wote wanaohitaji kujiunga kwa ajili ya kufanya udahili.    

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG