BANDA MEDIA BLOG

NANE-NANE DODOMA KUNA MAMBO, UDOM YAJA NA MVINYO (WINE) ULIOTENGENEZWA NA ASALI

 

Mwananchi akiangalia Wine ya Asali na Zabibu, iliyobuniwa na wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma wakati alipotembelea Banda la UDOM kwenye maonyesho ya Kimataifa Nanenane Nzuguni.

.....................

NA JOHN ISRAEL, NANE – NANE DODOMA

KWENYE maonyesho ya Wakulima na Wafugaji yanayofanyika Kimataifa katika viwanja vya Nane – nane Nzuguni jijini Dodoma kuna mengi ya kujifunza, leo nimepata nafasi ya Kutembelea Banda la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), na kujionea Mvinyo uliotengenezwa kwa asali ya Nyuki

Mtaalm wa Maabara Idara ya Baiolojia Ndaki ya Sayansi na Hisabati, Aichi Ofolo Mmbando, akiongea bandani hapo amesema WINE hiyo imevumbuliwa na Wanafunzi wa Baiolojia wanaosoma chuoni hapo.

“uvumbuzi huu wa wine ya asali na zabibu uliofanywa na wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma, unaiongezea ubora Zaidi wenye kumfaa mtumiaji kwani anapata virutubisho vya aina mbili kwa wakati mmoja”, amesema Mmbando  

kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo hicho Rose Joseph, amesema amefurahishwa na mwitikio mkubwa wa Wananchi wanaotembelea banda la Chuo hicho kwa ajili ya kujionea bidhaa, kupata elimu ya masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kulima kilimo cha kisasa, kupima afya pamoja na ushauri wa chakula tiba ili waweze kuboresha maisha yao.

amesema tangu maonesho hayo yaanze banda hilo limekuwa na idadi kubwa ya wananchi kwa ajili ya kupata elimu ambayo ni msaada katika kutatua changamoto zinazowakabili.

Bi. Joseph amesema kuwa watanzania kwa sasa wameelimika kwani wamekuwa na hamasa ya kujifunza ikiwemo kuacha ulaji holela na kwenda katika ulaji wenye manufaa ambao utawasaidia kuboresha afya ili kupunguza maradhi yanayotokana na mfumo wa maisha ya kila siku.

“Wananchi wana mwamko wa kujua afya zao katika masuala ya maambukizi ya virus vya ukimwi ili waweze kujua namna ya kuishi kama watakuwa na maambukizi pamoja na kuchukua tahadhari” amesema Bi. Joseph.

Amesema kuwa elimu imeendelea kutolewa na wataalam katika banda la Chuo Kikuu Cha Dodoma, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi wa kulinda afya zao.

 

Wanafunzi wa UDOM, Idara ya Sanaa Taaluma za Habari Ndaki ya Insia na Sayansi za Jamii wanaochukua Shahada ya awali katika sanaa za maonyesho na Filamu, wakitoa Burudani ya Ngoma katika viwanja vya maonyesho ya Nanenane 2024, Nzuguni jijini Dodoma

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG