.................
NA JOHN ISRAEL, NANE- NANE DODOMA
TAASISI ya Southern Highlands Tree
Growers Association. (SHTGA) inayofanya shughuli zake Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania yenye makao
yake makuu mkoani Njombe katika
jitihada zake kuboresha hali ya uchumi kwa vikundi wanachama wake inajuvunia
kuwezesha zaidi ya wanawake 40 wasusi wa vikapu.
SHTGA Kupitia mradi wake unaofadhiliwa na
Shirika la Kimataifa la Kimaendeleo la WE-EFFECT , Iimewawezesha wanawake wasusi
wa vikapu wa nyanda za juu kusini kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali ya kuongeza
ubora na thamani katika bidhaa hiyo ya vikapu mitindo vya mbalimbali
Mary Uswege (Meneja miradi – SHTGA anesema Taasisi hiyo imekuwa ikitoa Elimu ya
ujasiriamali na masoko ikiwa ni pamoja na kuwatafutia masoko yenye tija , ndani
na nje ya nchi.Pia, kupitia mradi huo wanawake hao wamepata fursa ya kushiriki
katika maonesho ya kimataifa ya kilimo (Nanenane :2024) yaliyofanyoka Kitaifa
katika Viwanja vya Nanenane vilivyopo Nzuguni, Jijini Dodoma yalihusisha sekta
mbalimbali ikiwemo Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.Ikiwa ni fursa nzuri kwa wanawake
hao kuweza kujifunza na kufahamiana na wadau mbalimbali wa sekta hizo, Sanjari
na kupanua wigo wa masoko ya bidhaa zao.
Meneja miradi kutoka Taasisi ya SHTGA Bi.
Mary Uswege anasema, mpaka sasa wameshaanza kugusa masoko ya Nje, kutokana na
ubora wa bidhaa zao, Idadi kubwa ya wateja iliyowafikikia katika masoko ambayo
wahusika waliona bidhaa zeo kwenye ukurasa wao wa Instagram inayofahamika kama
@fn_handmadebasket.
amesema Kupitia mafunzo yaliyotolewa kwa
wanawake hao wameweza kusuka vikapu vyenye ubora wa hali ya juu katika mitindo
mbalimbali yenye ladha na muonekano wa asili na ule wa kisasa vikiwemo vikapu
vya kubebea kompyuta mpakato (Laptop bag), vikapu vya maua na urembo pamoja na
mikoba ya kike, ambayo humpatia mtumiaji wa vikapu hivyo unadhifu wa kipekee.
Ameongeza kuwa, “kama SHTGA tunajivunia
kuwawezesha wanawake hawa kutengeneza vikapu vyenye ubora vinavyokidhi
mahitaji ya soko la hapa Tanzania lakini pia la nje”,
Ameeleza, shughuli hizi ni za kiutamaduni na
endapo wakiulizwa wasusi hao, walivyopata ujuzi husema walifundishwa na Bibi,
Mama na Shangazi zao. Hivyo; pamoja na Taasisi kuwaongezea maarifa hayo na
kuwawezesha kupata kipato pia wanahakikisha utamaduni huo unatunzwa na
kurithishwa vizazi na vizazi.
Aidha, amewapongeza wanawake hao, wasusi
wa vikapu kwa ustadi wa kipekee katika kutengeneza vikapu hivyo.Na kuongeza
kuwa, kwa sasa wanawake Zaidi ya 40 wananufaika na kupata kipato kutokana na
kuuza vikapu kwa bei ya thelathini elfu hadi arobaini na tano elfu(30,000-45,000)
kwa kila kikapu ikilinganishwa na bei ya awali kabla ya vikapu hivyo kuongezewa
thamani ambapo kiliuzwa kwa Elfu kumi hadi Elfu kumi na
tano(10,000-15,000) kila kimoja abapo Shughuli hizo za uuzaji wa vikapu
vimewawezesha wanawake hao kupata kipato na kuboresha maisha yao.
Ameongeza kuwa jamii kiujumla wameweza kujenga nyumba ,kusomesha watoto,
wamepata mitaji na kuwekeza katika shughuli nyingine ili kuongeza kipato kama
vile, biashara na kilimo hivyo kuongeza usalama wa chakula.
Bi. Mary Uswege
(Meneja miradi – SHTGA) amehitimisha kwa kufafanua kuwa “ Wanawake
walionufaika chini ya mradi huu ni wale walio katika vikundi wanachama wa
Muungano wa wakulima wa miti Nyanda za Juu Kusini.”
Meneja Miradi wa taasisi ya SHTGA Mary Uswege akimuelezea Rc. Senyamule jambo kuhusu ususi wa vikapu bora unaofanywa na wanawake wa nyanda za juu kusini wanaoshiriki maonyesho ya Nanenane 2024 jijini Dodoma.