BANDA MEDIA BLOG

WE EFFECT LAJIVUNIA KUWAFIKIA WAKULIMA LAKI 120 TANZANIA

 


                                          ......................

               NA JOHN BANDA, DODOMA

MAONYESHO ya Wakulima na Wafugaji ambayo yamekuwa yakionyesha zana mbalimbali za Kilimo na Mifugo yamehitimishwa kitaifa hivi karibuni na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma ambapo alitumia nafasi hiyo kuzindua miradi mbalimbali ya sekta hizo muhimu hapa nchini

Katika maonyesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Nane-nane Nzuguni jijini humo, yalihusisha mashirika na makapuni mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kuonyesha vumbuzi na bunifu ambazo zikitumiwa kama zilivyokusudiwa ni wazi kuwa taifa letu litapiga hatua za kimaendeleo katika kila eneo hasa katika Mifugo na kilimo.

Ndani ya Maonyesho hayo Kumekuwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la  WE EFFECT, lenye makao yake makuu huko nchini Swiden ambalo linafanya kazi katika nchi Zaidi ya 20, katika mabara ya Asia, Latini Amerika na Africa Mashariki ambapo Ofisi za kanda zipo Nairobi Nchini Kenya likiwa na uzoefu wa miaka 60, tangu lilipoanza shughuli zake.

Meneja wa Shirika hilo Tanzania, Frank Adimba  anasema lengo kubwa la Shirika hilo ni Kuondoa Umasikini kwa wakulima na makundi mengine kupitia vyama vya ushirika na kwamba hadi sasa linafanya kazi na vyama Pamoja na taasisi 13 hapa nchini, ambapo linajivunia kuwafikia watu laki 120 wanaojishghulisha na kilimo.

“hapa nchini tayari tunafanya kazi na vyama vya ushirika 13, tukiwa tumewafikia wakulima laki moja na elfu ishirini (120,000) huku asilimia 54 wakiwa ni wanawake”, amesema

Amesema kuwa malengo makubwa ni kuhakikisha kuwa walengwa wanakuwa na Maisha bora Pamoja na haki ya upatikanaji wa chakula (USALAMA WA CHAKULA) kwa kuwajengea uwezo kupitia Vyama vyao vya ushirika.

Anasema katika vyama hivyo vya ushirika Pamoja na taasisi za kiraia ambazo wanafanya nazo kazi mara nyingi zimekuwa zikilegzlega kwenye uongozi, hasa kwenye kuwasaidia wakulima kufikia malengo,  hivyo Shirika huwawezesha kuweka mifumo thabiti ya Uongozi, Sera Bora kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanasima kitaasisi.

Anasema Lengo lingene ni kuwa wanahakikisha wanaimarisha mifumo ya Chakula, kupitia Kilimo kwani wadau wao ni wakulima kwa kuanzia Uzalishaji, Usindikaji mpaka uuzaji wa bidhaa mbalimbali ndani ya mnyororo wa thamani.

Meneja huyo Anesema shirika linawajengea uwezo wakulima wa kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kujenga nyumba bora za kisasa, kwani  si busara Mkulima akazilisha na kuuza huku akawa bado anaishi kwenye nyumba isiyo na hadhi.

WE EFFECT kupitia Programu yake ya Ujenzi wa nyumba bora vijijini kwa sasa linajivunia Zaidi ya nyumba 5000 zilizojengwa na wakulima wa Tanzania kutokana na kuchangishana wakichagizwa na huduma ndogo ya za kifedha

“tunawafundisha kupitia mkondo wa huduma ndogo za kifedha, wanafikia hatua ya kuwekeza na kuwezeshana kwa kuchangishana kiasi cha kufikia hatua ya kujenga nyumba ambapo sasa tunajivunia nyumba bora 5000 tayari zimeshajengwa na wakulima hapa tanzania”, amesema

USHIRIKA

Aidha Meneja Adimba amewataka Wakulima na Makundi mengine kujiiunga kwenye Vyama vya ushirika ili wakatengeneze Nguvu na Sauti ya Pamoja ambayo itawafanya kusikika kama ilivyo Nchii Kenya ambako makundi mbalimbali yakiwemo Bodaboda, Mbogamboga, madereva wa matatu na mengine mengi yanaungana Pamoja.

“ushirika unawaleta watu Pamoja, wanakuwa na nguvu na sauti ya Pamoja ya kuweza kueleza mambo yao yakasikika lakini pia kuongeza uzalishaji, kwani mkono mmoja haupigi makofi,

Pia ukitaka kwenda haraka nenda peke yako, lakini ukitaka kwenda mbali kwa uhakika nenda na wenzako mtafika salama lazima mkiwa kwenye ushirika mtakidhi mahitaji ya soko”, amesema na kuongeza

Ameongeza kuwa “mkiwa Pamoja mtapanga bei ya Pamoja Pamoja na kupata soko la uhakika kunakosababishwa na kuuza kwa Pamoja”,

pia amesema Benki Kuu ya Ushirika ya nchini Kenya ndiyo inayoongoza nchini humo kwani wakulima wote wana hisa hivyo huweka na kukopa kwa ajili ya kuendeza fani yao, hivyo kwa Tanzania amesikia hivi karibu kutazinduliwa Benki ya KCBL ambayo amesema itakuwa mkombozi kwa wakulima na makundi mengine yatakayokuwa na hisa.

Shirika hilo linawezesha vyama vya ushirika vinavyotoka na wakulima, wafugaji, walinaji wa asali, wasusi wa vikapu, wakusanya maziwa na kuyasindika na kuyauza, wachongaji wa zana za mikono Pamoja na wengine mengi.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG