BANDA MEDIA BLOG

WAANDISHI JIJINI DODOMA WALIBANA MASWALI JESHI LA POLISI KUHUSU KIFO CHA MAN'DOJO

 

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SACP Anania Amo akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 13,2024 jijini Dodoma

NA JOHN BANDA, DODOMA

WAANDISHI wa Habari walibana kwa maswali Jeshi la Polisi mkoni Dodoma kuhusu kifo cha mwanamuziki wa Bongo Fleva  Josephas Michael Maarufu Man'dojo lenyewe latoa ufafanuzi huku likitoa onyo kwa wanaojichukulia sheria mkononi.

Man'dojo ambaye enzi za uhai wake alipata kutamba na vibao kadhaa kikiwemo Nikupe Nini Honey akishirikiana na  Domokaya, Taarifa za Kifo Chake zilizagaa kwenye Mitaandao mbalimbali ya kijamii Pamoja na Baadhi ya vyombo vya Habari Agosti 11, mwaka huu,

Akitoa Ufafanuzi hii leo agosti 13,2024 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Anania Amo mbele ya Waandishi wa Habari amesema Majira ya saa 6 mchana wa siku hiyo Mandojo alipoteza Maisha wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospital ya Rufaa ya Mkoa huo.

Akifafanua Zaidi amesema saa 11 alfajiri ya Siku hiyo Mandojo ambaye ni mkazi wa Nzuguni B, Jijini humo alikutwa katika moja ya chumba Kilichopo ndani uzio wa Kanisa la  Rc. Parokia ya Watakatifu Wote ambapo mlinzi alishtushwa na sauti za Mbwa aliyekuwa akimbwekea na ndipo akaingia chumbani humo.

“mlinzi baada ya kusikia mbwa akibweka ndipo alipoenda kuangalia kuna nini ndipo alipogundua kuna mtu ndani ya chumba hicho ambapo akapiga kelele kuita watu wamsaidie ambapo waumini waliokuwa wanaingia ibadani misa ya kwanza siku ya Jumapili wakafika wakaanza kumshambulia Mandojo kwa Pamoja”, amesema

Aidha Kaimu Kamanda huyo amesema jeshi hilo lina mshikilia Kwa Mahojiano kuhusiana na Tukio hilo Mlinzi huyo Rafael Keneth.

Kaimu huyo ambaye ni Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi amesema Watu wengine Wawili Franco Filibert (29) Muhaya na Ramadhan Abeid (27) Mzgua wameuawa kwa kupigwa katika maeneo mbalimbali ya miili yao na kisha wakachomwa moto ndani ya Gari yao huko Ibihwa wilayani Bahi.

Amesema watu hao waliotoka Dodoma mjini walifika ibihwa wakielekea katika kitongoji cha  Juhudi kupeleka Token za mchezo wa kubahatisha majira ya saa 4 usiku wa Agosti 8, 2024  wakiwa na gari yenye namba za usajili T 583 BEW aina ya Toyota Crester ambapo hawakuendelea na safari kutokana na barabara kutopitika ikabidi wamtume wenzao kupeleka tokeni hizo kwa Bodaboda.

“wapita njia walilitilia mashaka gari hilo kutokana na kuegeshwa katika eneo hilo kwa Muda mrefu, ndipo wakaitana na kuanza kuwashambulia kisha kulichoma gari hilo huku watu hao wakiwa ndani hali iliyosababisha kifo chao miili yao imehifadhiwa katika chumba cha kuhfadhia maiti katika hospital ya wilaya ya Bahi”, amesema

Baada ya taarifa hizo maswali ya waandishi wa Habari yakaibuka, wakita kujua Kwanini Afisa Mtedaji huko Ibihwa alizuia Gari ambalo lilichomwa moto lisipigwe Picha lakini pia Matukio ya wananchi kujichulia sheria Mkono yatakoma lini lakini pia jeshi hilo lina mkakati gani kwa ajili ya Usalama wa Raia na mali zao maana mara nyingi askari wa Doria wamekuwa wakifika kwenye mitaa kutokana na matukio?

Kaimu Amo akijibu amesema Jeshi hilo halikumuagiza Mtendaji huyo kuzuia waandishi wasifanye kazi yao katika eneo la tukio, kuhusu wananchi kujichukulia sheria Mkoni amesema jeshi hilo limekuwa likipita katika taasisi za dini, mashuleni na kwenye mikusanyiko kutoa elimu na kuhusu Doria “tuna askari wachache hivyo hawawezi kuwa kila sehemu kwa wakati mmoja hivyo wananchi wahakikishe wanatoa ushirikiano kwa kuanza kujilinda wao kabla ya polisi kufika.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG