BANDA MEDIA BLOG

DCEA YATOA ELIMU KWA WADAU WA MAENDELEO YA VIJANA JIJINI ARUSHA

                   

         

                                                       Na Prisca Libaga Arusha

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 30.08.2024 imetoa elimu juu ya tatizo la dawa za kulevya kwa wadau na taasisi zinazofanya kazi na vijana katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha jijini Arusha.
Jumla ya wadau 152 kutoka taasisi/asasi mbalimbali walishiriki kikao hiko kilichokuwa na lengo la kujadili Sera ya Vijana iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Baada ya washiriki hao kupata elimu, wameahidi watafikisha ujumbe huo kwa vijana kama sehemu yao ya kushiriki katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya mkoani Arusha.   

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG