BANDA MEDIA BLOG

YANGA SC YATUMA SALAMU NZITO KWA SIMBA SC BAADA YA KUICHAPA JKT TANZANIA 5-0


 Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans Sports Club, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliochezwa leo, Februari 25, 2026, kwenye Dimba la KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Zimbwe Jr dakika ya 7, Depu dakika ya 60, Mudathir dakika ya 63, Dube dakika ya 85, huku bao la tano likifungwa na Khamis dakika ya 89 na kuhitimisha wimbi la ushindi.

Ushindi huo ni sehemu ya ujumbe thabiti kwa wapinzani wao, Simba Sports Club, kabla ya Dabi ya Kariakoo itakayofanyika Jumapili, Machi 1, 2026.

Mashabiki wa Yanga baada ya ushindi huo walionekana wakiimba, “Bado Simba! Bado Simba!” kuelekea mechi ya Dabi ya Kariakoo itakayofanyika Jumapili, Machi 1, 2026, Visiwani Zanzibar.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG