BANDA MEDIA BLOG

MKUMBO AONGEZA NGUVU USHIRIKIANO WA UWEKEZAJI TANZANIA NA SHANDONG, CHINA

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Biashara wa Jimbo la Shandong, Mheshimiwa Wang Lei, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kimkakati pamoja na namna ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao walijikita katika kuhamasisha uwekezaji kati ya Tanzania na Jimbo la Shandong nchini China, hususan katika sekta muhimu za maendeleo. Prof. Mkumbo ameridhia mapendekezo na makubaliano yaliyowasilishwa, ikiwa ni pamoja na kuanzisha na kuimarisha ushirikiano katika sekta za kimkakati kama vile viwanda, madini, kilimo na utalii.

Aidha, mbali na kikao hicho, Prof. Kitila alifanya mazungumzo ya kina na wawekezaji mbalimbali wanaotarajia kuwekeza nchini Tanzania. Miongoni mwao ni wawekezaji wakubwa katika sekta ya saruji kutoka Kampuni ya Anhui Conch Cement Co., Ltd, wakiongozwa na Bw. Terry Chu, ambao wamevutiwa kuwekeza Tanzania na ndio nchi ya kwanza kwao katika nchi za Afrika.

Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada endelevu za Serikali za kuvutia uwekezaji wa kimataifa, ambapo inahusisha makongamano na vikao vya kimkakati vinavyolenga kukuza na kuendeleza sekta ya uwekezaji nchini.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG