NA JOHN ISREAL, DODOMA
MKURUGENZI wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO),
Dkt. Venancy Mwase amesema kitendo cha Waumini kukutana katika Mfungo wa
Ramadhan na Kwaresma ni funzo toka kwa Mungu linalomaanisha Watanzania wote ni
wamoja.
Dkt. Mwase ametoa kauli hiyo kwenye tukio la
kuwafutarisha makundi mbalimbali wakiwemo Wajane, Wagane, Watoto wanaoishi bila
huduma za wazazi, watu wenye ulemavu na Washirika wenza wa Biasahara ya Nishati
saafi, wakiwemo wanawake na Samia mkoa
wa Dodoma
“tangu nimekuwa sijawahi kuona watu wa dini hizi
kubwa kufunga kwa wakati mmoja, watanzania ni wamoja, Tanzania siyo nchi ya
udini, Mungu ametupa funzo ndiyo maana leo tumekaa tunakula pamoja,
hii mimi siiti Futari naita chakula cha Upendo, watu
wa makundi mbalimbali wamekutana wamekaa na kula pamoja huu ni upendo ulioje
unaojengwa na shirika lenu la stamico na niwaambie tu Futari hii itaendelea
kila mwaka”, amesema
aidha amesema shirika hilo linalohudumia wachimbaji
wadogo wa madini hapa nchini litaendelea kuyawezesha makundi mbalimbali katika
uchumi shirikishi ikiwa ni pamoja na mpango wa kuwawezesha Watoto wenye
mahitaji maalum…
Mgeni Rasmi
katika hafla hiyo, Katibu Tawala msaidizi anayeshughulikia Uwekezaji, viwanda
na Biashara mkoa wa Dodoma Mwajabu Nyamkomori, amelipongeza shirika la STAMICO
ambalo limewawezesha wachimbaji wadogo wa madini kupiga hatua za kimaendeleo.
Aidha pongezi na shukurani nyingine zimetoka kwa
mwenyekiti wa Wanawake na Samia Fatuma Madidi, pamoja na Mkurugenzi wa Foundation
for Disabilities Hope ambao ni washirika wenza katika Biashara ya Nishati safi kwa
kushirikiana na STAMICO.
Walioshiriki katika Futari hiyo ya Ramadhan na
Kwaresma ni pamoja na makundi ya watoto Yatima kutoka ntyuka, Kisasa na Miyuji,Watu
Walemavu wa ngozi chini FDH (Foundation
for Disabilities Hope), walemavu wa viungo kutoka kituo cha Samaria Hombolo, chini
ya Shivyawata, wajana, wagane, pamoja na wanachi wa kawaida