BANDA MEDIA BLOG

Rais Putin aapa kujibu shambulio la Ukraine kwenye shule Luhansk

 


Na:


Idadi hiyo imethibitishwa na mamlaka inayoungwa mkono na Urusi kwenye eneo hilo.

Kulingana na gavana wa jimbo la Luhansk linalokaliwa na Urusi, Leonid Pasechnik, watu 38 wamejeruhiwa kwenye shambulio hilo ambapo wanafunzi 11 hawajulikani walipo.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amelaani shambulio la ndege isiokuwa na rubani ya Ukraine kwenye bweni la shule hiyo katika Mji wa Starobilsk kwenye jimbo la Luhansk.

Ukraine kwa upande wake inasema haikulenga maeneo ya kiraia kwenye eneo hilo lakini ilishambulia kituo cha Urusi cha kuhifadhi droni
Ukraine kwa upande wake inasema haikulenga maeneo ya kiraia kwenye eneo hilo lakini ilishambulia kituo cha Urusi cha kuhifadhi droni REUTERS - Pavel Klimov

Putin amesema amewaagiza wanajeshi wa nchi yake kujiandaa kulipiza kisasi.

Ukraine kwa upande wake imekanusha kuwalenga raia kwenye shambulio hilo, ikisema ilishambulia kituo cha kuhifadhi ndege zisizo na rubani za Urusi kwenye Mji wa Starobilsk.

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi nayo imesema wahusika wa shambulio hilo wataadhibiwa vikali.

Rais wa Urusi Vladmir Putin amewataka wanajeshi wake kujiandaa kujibu shambulio hilo.
Rais wa Urusi Vladmir Putin amewataka wanajeshi wake kujiandaa kujibu shambulio hilo. REUTERS - Pavel Klimov

Mji wa Starobilsk upo kilomita 65 sawa na maili 40 kutoka katika eneo ambalo mapigano yamekuwa yakiripotiwa mashariki mwa Ukraine.

Wanajeshi wa Urusi waliuchukua Mji huo mwaka wa 2022, muda mfupi baada ya kuanzisha kikamilifu uvamizi wake nchini Ukraine.

Jimbo la Luhansk kwa sehemu kubwa linakaliwa na wanajeshi wa Urusi, Moscow ikisema ni sehemu ya himaya yake.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG