DIWANI wa kata ya Iyumbu Jijini Dodoma Sadiki
Mponyamili ametembelea na kujionea shuhuli zinazofanywa na Wanakikundi cha
Wachimba kokoto cha NZINJE IYUMBU na kubaini eneo lao la Leseni limepimwa
viwanja huku wakifungiwa mashine yao ya kukusanyia Ushuru (POS).
Mwenyekiti wa Mtaa wa Iyumbu Nasson Lugunyale amesema
kutoakana na hali hiyo kumesababisha familia nyingi kuishi Maisha ya Taabu
kwani wengi wao walitegemea shuhuli hiyo kutunza familia zao kwa zaidi ya miaka
43.
“inashangaza sana wamefungiwa kutofanya kazi zao za
uchimbaj wa madini wakati leseni yao bado inasoma, ambapo sasa hali za familia
za wachimbaji hao zaidi ya 100 ni tete kwani wanashindwa hata kuwalipia ada Watoto
wao pamoja na maendeleo mengine” amesema
Diwani Mponyamilia akichapisha kwenye ukurasa wake wa
Facebook ameandika, “Leo nimetembelea na kuwasikiliza Wana kikundi
wanaojihusisha uchimbaji madini ujenzi (kokoto,mawe)... KIKUNDI CHA NZINJE
IYUMBU
Nimesikiliza changamoto zao Ili kuona ufumbuzi zaidi.
Moja kati ya changamoto yao ni kuwa mashine Yao ya
kukata ushuru (POS) imefungwa , mashine hiyo ilifungwa huku kukiwa na madai
kuwa hawaruhusiwi kuendesha shughuli hiyo ya uchimbaji madini ujenzi lkn pia
nmeweza kujua kwamba wanayo LESENI inayofanya kazi (active licence up to
2027),huku kero Yao kubwa kwann wamefungiwa mashine ambayo ingesaidia kupata
mapato serikalini na kwamba jambo hili nimelipokea kwa utatuzi zaidi.....
Lakini pia wameibua hoja ya Eneo Hilo kudai limepimwa
kinyemela bila wao kuhusishwa na kwamba Eneo Hilo pamoja na shughuli ile lkn ni
Eneo ambalo wamekuwa na shughuli hyo tangu mwaka 1983 na Kisha 2013 wakaweza
kupata LESENI Eneo Hilo,nimeahidi kulifanyia kazi
Mwisho wamefurahi kuona kiongozi wao amewatembelea
kwani haikuwahi kutokea kiongozi wao kwenda Eneo lao la kazi na kuweza
kuwasikiliza, zaidi wamekuwa wakiwasilisha tu changamoto zao serikali za
mtaa... ",ameandika Mponyamili




