MKUTANO wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma unaendelea katika ukumbi wa halmashauri kwa ajili ya kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 unaoishia 30 Juni 2025.
Mkutano huo unalenga kupitia na kujadili hoja pamoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kuimarisha uwajibikaji, usimamizi wa rasilimali na utoaji wa huduma kwa wananchi.


