BANDA MEDIA BLOG

CCM, KIMEMPOTEZA BALOZI MAKINI NA MWADILIFU- KUNAMBI

Na Barnabas Kisengi Dodoma 

Julai 05. 2026

Mamia ya waombolezaji wamejitokeza kwenye ibada ya kumwaga aliyekuwa mjumbe wa shina namba 5 tawi la CCM kilimani Balozi Juma saigwa Machaka  ibada iliyofanyika katika kanisa la Anglican parishi ya chinyoyo kata ya kilimani Jijini Dodoma 

Ibada hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Juma Saigwa Machaka imeongozwa na katibu wa umoja wa wanawake UWT Tanzania Suzani Kunambi aliyeambatana na katibu wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma Pilli Mbaga na viongozi wengine wa chama cha mapinduzi na serikali.

Akitoa salamu za rambirambi kwa waombolezaji waliojitokeza kwenye ibada hiyo katibu wa umoja wa wanawake UWT Tanzania Suzani Kunambi amesema chama cha mapinduzi kimempoteza Balozi makini, mwadilifu na mzalendo wa kweli.

Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma Pilli Mbaga amesema Juma saigwa Machaka alikuwa Balozi mwadilifu licha ya kuwa mjumbe wa shina namba 5 ambalo viongozi wengi wa chama na serikali wamakuwa wakiishi katika shina hilo.

"Tukisema tumuelezee Balozi Juma saigwa Machaka hapa hatutamaliza kwakuwa alikuwa mwadilifu na mzalendo na mcheshi kwa kila mtu juma alikuwa anafuatilia na kujua watu wake wote wa shina lake alikuwa hataki kuona mgeni amefika bila kujitambulisha kwenye shina lake na alihakikisha swala la usalama katika shina lake uko salama siku zote"amesema katibu Pilli Mbaga 

Akitoa mahubiri katika ibada mchungaji wa kanisa la Anglican church parishi ya chinyoyo mch  amesema kuwa sisi wanafamilia hapa Duniani tunapita tu hivyo tuige mema ya juma licha ya kujitoa katika shughuli za chama cha mapinduzi pia alitumia muda wake mwingi kujitoa katika kanisa na alikuwa Mzee wa kanisa.

Kwa upande wao wenyeviti wa mitaa minne ya kata ya kilimani wamesema wamempoteza kiongozi mahiri sana na mwadilifu na mchapakazi na mzalendo aliyekuwa akijitoa kwenye kazi za chama na serikali bila kuchoka wala kujali muda wake hakika wamepata pengo kubwa sana.

Akisoma wasifu wa marehemu Balozi Juma saigwa Machaka katibu wa chama cha mapinduzi kata ya kilimani Ramadhani Ramadhani amesema juma amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu katika hospital ya Benjamini mkapa na Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa muda marefu hadi umauti ulipo mkuta alfajiri ya Julai 04 2026 nyumbani kwake kilimani mtaa wa Nyerere marehemu Juma saigwa Machaka ameacha mjane moja na watoto wanne.

Marehemu Balozi Juma saigwa Machaka alizaliwa Mei 01 1965 na amefariki Julia 04 2026 na amezikwa Julia 05 2026 katika makabiri ya familia yaliyoko katika kijiji cha msanga wilayani chamwino mkoani Dodoma ambapo mazishi hayo yameudhuriwa na mamia ya Wananchi na viongozi wa Chama cha mapinduzi CCM na serikali.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Mwisho











 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG