BANDA MEDIA BLOG

BEKI MPYA NATHANIEL CHILAMBO ASAINI SIMBA KWA NJIA YA MIUJIZA



 Beki mpya wa Simba SC, Nathaniel Chilambo, amefunguka kuhusu nafasi kubwa ya imani ya Dini ya Kikristo katika maisha na safari yake ya mpira, akieleza kuwa amepewa jina la Nathaniel kutokana na babu yake aliyekuwa Askofu Mkuu. Chilambo amebainisha kuwa amelelewa katika mazingira ya kidini sana na yeye mwenyewe ameokoka na kumchagua Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa maisha yake, jambo linalomfanya aweze kufanya ibada na kumtanguliza Mungu katika kila jambo analofanya.

​Pia amefichua muujiza uliotokea kabla ya usajili wake kwenda Msimbazi, ambapo akiwa kwenye maombi na baba yake wa kiroho, alitabiriwa kuwa kuna neema ya klabu fulani kubwa Mwenyezi Mungu anataka kuiachilia kwenye maisha yake. Siku chache baadaye alipokea simu kutoka kwa uongozi wa Simba SC kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kusaini mkataba, jambo ambalo analiona kama baraka na muujiza mkubwa kutoka kwa Mungu kuelekea kuhudumia klabu hiyo kubwa.


​Unazungumziaje imani na mtazamo huu wa Nathaniel Chilambo anapoingia Msimbazi? Dondosha maoni yako!

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG