BANDA MEDIA BLOG

JICHO LA MITANDAO YA KIJAMII KWENYE MCHEZO WA YANGA NA GABORONE LIGI YA MABINGWA

 


Katika Mchezo huo uliopigwa septemba 12,2026 katika uwanja wa Chamanzi Dsm, Young Africans imefanikiwa kuifunga Gaborone United kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kufuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo. Hata hivyo, licha ya ushindi huo, baadhi ya mashabiki wa Yanga hawakuridhishwa na mwenendo wa kocha wao, Manqoba Mngqithi, hasa katika eneo la mabadiliko ya wachezaji.

Uamuzi wa kumtoa Aziz Ki uliibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki, huku baadhi yao wakiona kuwa timu ilikosa ubunifu baada ya mabadiliko hayo. Baadhi ya mashabiki wameenda mbali zaidi kwa kutaka kocha huyo aondolewe, wakidai ameshindwa kuingia kwenye mfumo unaompa nafasi na kutumia ipasavyo uwezo wa Aziz Ki.
Hata hivyo, pamoja na malalamiko hayo, Yanga imefanikiwa kupata ushindi na kusonga mbele katika mashindano hayo. Sasa Wananchi wanaelekeza nguvu zao kwenye maandalizi ya michezo inayofuata.

...
YANGA KWA STYLE HII SIWAONI MBALI
Well, ilikuwa mechi nzuri sana Yanga wamecheza vizuri, lakini Gaborone United wametupa surprise ya aina yake. Wamecheza mpira wa kitabuni kabisa pasi nyingi zenye macho, maelekezo mazuri na nidhamu ya kiufundi. Kitu walichokosa zaidi ni ubunifu wa mwisho.
Kwa upande wa Yanga, si kwa ubaya, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Hii ni michuano ya Klabu Bingwa Afrika, sehemu ambayo kosa dogo tu linaweza kukugharimu na mpinzani akacheka na nyavu.
Yanga bado wanaonekana kuwa na baadhi ya makosa madogo madogo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi mapema kabla hayajawa tatizo kubwa.
Lakini kule mbele nako kuna jambo la kujiuliza… Yanga wamekosa nafasi nyingi sana nafasi kama zile kwenye mechi za kiwango hiki zinapaswa kutumiwa vizuri.
Kwa ujumla, mchezo ulikuwa mzuri, lakini ujumbe ni mmoja: Yanga bado wana kazi ya kuongeza umakini, ubunifu na umaliziaji.
Paul Kanuti
......

Mchambuzi wa Wasafi FM, Dulla Heavyweight, amesema kuna siku watu watagundua yeye ni mtu wa aina gani, akisisitiza kuwa soka linahitaji wachambuzi wa aina yake kuongezeka zaidi. Dulla amesema amekuwa akisimamia ukweli na kufanya utafiti kabla ya kuzungumza, akidai kuwa tangu Manqoba Mngqithi alipotambulishwa Yanga, yeye alikuwa miongoni mwa wachambuzi waliokuwa na mtazamo tofauti kuhusu uwezo wa kocha huyo.
Amesema wakati wengi wakimsifia Mngqithi kutokana na wasifu wake wa kufanya kazi Mamelodi Sundowns, yeye aliona ni kocha wa kawaida aliyepata mafanikio akiwa chini ya Pitso Mosimane na Rulani Mokwena, huku akidai mara mbili timu zilipoachwa mikononi mwake hakufanya vizuri. Dulla amesema sasa tayari kuna kundi kubwa limeanza kuwa na mashaka kuhusu uwezo wa Mngqithi, akisisitiza kuwa ukweli unaweza kuchelewa kuonekana, lakini mwisho wa siku hujitokeza.

....

MOJA YA PERFORMANCE MBAYA ZAIDI KUWAHI KUISHUHUDIA YA YANGA! 😳⚽
Moja ya performance mbaya kuwahi kuishuhudia ni hii ya leo ya Yanga. Kuna namna ambavyo kila siku tunaambiwa kuhusu ubora wa timu hii, lakini ukiangalia uhalisia hasa kwenye michezo ya kimataifa, unaanza kujiuliza:
Kweli huyu ndiye Bingwa wa Ligi Kuu tunayemtegemea kuiwakilisha Tanzania kimataifa?
Yanga imefanikiwa kufuzu, hilo halina ubishi. Lakini pamoja na kufuzu, performance yao leo imeacha maswali mengi kuhusu safari yao huko waendako.
Mechi ya leo dhidi ya Gaborone ilikuwa ya kushtua. Kwa namna mchezo ulivyokuwa, ni kama Yanga walikuwa hatua moja tu kutoka kwenye kutibua mambo yote.
Kwa lugha rahisi tunaweza kusema:
“JINI KATOKA, LAKINI MGANGA YUPO HOI!” 😂
Yanga imefuzu kwa aggregate ya 3-2, lakini kama timu itacheza kwa kiwango hiki katika hatua zinazofuata, itakuwa na kazi kubwa sana mbele yake.
Kufuzu ni jambo moja, lakini performance na uwezo wa kushindana katika hatua kubwa ni jambo lingine kabisa.
Swali la kujiuliza ni moja tu:
HII YANGA INAWEZA KWELI KUFIKA MBALI KIMATAIFA KAMA PERFORMANCE YAKE ITABAKI HIVI?

.......
Ukiangalia mchezo uliopita, bao la Gaborone lilipatikana baada ya Ibrahimu Bacca kupoteza umiliki wa mpira. Akalazimisha kupokonya mpira alioupoteza, akafanya faulo, ikazaa bao.
Leo tena...
Bakari Mwamnyeto alikuwa na nafasi ya kutoa mpira, akataka kugeuka, akajikuta anasogeza presha, akapoteza mali. Gaborone wakapiga pasi chache, goli likaingia.
Mabeki wa kati wa Yanga wamefanya makosa binafsi mara mbili mfululizo kwenye mechi moja kitu ambacho nyuma hawakuruhusu mabao
Mfano .....
Ukirejea takwimu kabla ya mchezo wa leo, Yanga ilikuwa imeruhusu mabao 4 katika mechi 10 zilizopita za nyumbani pekee.
Katika hatua hizi za awali, kuanza kuruhusu mabao mapema kunaweza kuwa sehemu ya mpinzani kumwambia, ukiwa unakuja kucheza na mimi, anza kunichunguza hapa kwenye safu ya ulinzi; ndipo nilipo na makosa zaidi.
Hatua ya makundi ina wapinzani ambao wanatafta udhaifu wako wautumie sasa kama kosa ni individual kama magoli yaliyofungwa saivi tafsiri yake mpinzani anayefanya research hato hangaika kuja kuifunga Yanga.
Manqoba lazima aboreshe eneo la ulinzi mara mbili zaidi.
✍️KALAMU YA USHAHIDI
.....
KABLA YA MCHEZO
Nguli wa habari na Gwiji wa Gaborone United TSHEPO MOLWANE anatamba kuwa wao kwa Tanzania Simba ndiyo wanaihofia zaidi kuliko Yanga.
Kwqhiyo mchezo wa leo lolote linaweza kutokea kwa sababu timu hizi hazitofautiani sanaa kiuchezaji mchawi mbinu tu.
Tshepo Amefika mbali zaidi kwamba Tanzania Simba SC ndiyo Timu tushio kimataifa kufananisha na Young Africans.
Yapi maoni yako mwananchi kwa mkongwe huyu wa Habari wa Gaborone?

....
POST
AMEANDIKA FARHAN JR
Nimesafiri nchi kadhaa Afrika kama Mwandishi nimeshuhudia matukio ya kihuni sana ambayo timu za Tanzania zinafanyiwa zikiwemo nchi ambazo ni kubwa kimpira Afrika lakini huoni Mashabiki wala Waandishi wao watapost hizo clip, kwao linapokuja suala la Klabu zao ni Uzalendo wa hali ya juu kifupi kuanzia Walinzi, Mashabiki mpaka Waandishi lao moja mtateseka sana na hakuna Ushahidi mtapata kwenda CAF kirahisi.
Leo hii Waandishi wetu wanachapisha Clip za matukio ya Stewards wa Yanga zaidi kuliko matukio ya Watswana, maana yake tumewasaidia CAF kupata usahidi na Yanga watahukumiwa inawezekana faini ya pesa ama vyovyote kuna muda tuachane na hisia, utofauti wetu na tuzitazame timu zetu kwa maslahi mapana ya Taifa na hatuwazi tuna AFCON hapo jirani tu, tunajipa picha ya KIHUNI.
Tunaweza kurekodi mambo yetu ya ndani ila sio International adhabu ni kali sana, ile clip ya Morocco walifanya vurugu hapo Mkapa mechi na Simba nilirecord Mimi na Afisa wa Simba aliombwa na CAF nimtumie original kama ushahidi na Jamaa walipigwa mvua sasa sisi leo tumerecord zetu na kupost ni ushahidi tosha.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG