BANDA MEDIA BLOG

MAASKOFU ANGLIKANA, WATEMBELEA FAMILIA YA HAYATI MAGUFULI NA KANISA CHATO


 Na Rev. Rev. Maiko Luoga – Chato

Maaskofu wa Dayosisi za Kanisa Anglikana Tanzania na wake zao, wametembelea makazi ya Familia ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yaliyopo wilayani Chato mkoani Geita.

Baada ya kuwasili katika makazi ya familia ya Hayati Magufuli Chato, Ijumaa Tarehe 28 Agosti 2026, Msafara huo ukiongozwa na Askofu Joseph Mgomi wa Dayosisi ya Ruaha mkoani Iringa aliyemwakilisha Askofu Mkuu Maimbo Mndolwa, Ulipokelewa na Mke wa Hayati Dkt. Magufuli, Janeth Magufuli.

Wakiwa mahali hapo Maaskofu na Msafara wao walishiriki Ibada fupi ya pamoja na Mke wa Hayati Magufuli ambae alishukuru Kanisa Anglikana Tanzania kwa kufika na kutoa Neno la Mungu kwa familia, kisha Maaskofu, walipata nafasi ya kutembelea na kuona Kaburi la Hayati Magufuli.

Ziara hiyo ilihudhuriwa na Ugeni wa Katibu Mkuu wa Ushirika wa Kanisa Anglikana Ulimwenguni, Askofu Antony Poggo na Maaskofu wateule wa Dayosisi za Zanzibar na Handeni pamoja na wake zao.

Aidha Msafara huo ulitembelea Kanisa la Mtakatifu Stephano Chato Dayosisi ya Biharamulo na kupokelewa na Waumini wa Kanisa hilo wakiongozwa na Kasisi Kiongozi Canon. Zacharia Kasela kisha kuona kazi za maendeleo ya Kanisa hilo.

Pamoja na kazi ya Injili waumini, wanaendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa Kanisa jipya pamoja na kuwahudumia watoto wanaotoka katika mazingira magumu kupitia Kituo cha Maendeleo ya Huduma ya Mtoto na Kijana.

Bi. Neema Karoly, Mratibu wa Kituo hicho alisema, lengo Kuu la Kituo, Kumkomboa mtoto na lindi la umaskini kupitia Jina la Yesu, kazi ambayo inaendelea kwa kushirikiana na ushirika wenza wa Compassion International Tanzania.

The Anglican Church of Tanzania (ACT) 

Dwt Habari







Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG