Mchezaji wa zamani wa Ufaransa na Liverpool Djibril Cisse hivi karibuni alikamatwa na polisi nchini Ufaransa kwa makosa hayo hayo yanayofanana na Benzema.
Cisse aliachiwa na polisi tarehe 13 kufuatiwa kukamatwa nyumbani kwake saa 12 asubuhi jijini Paris.
Leo hii sasa shirika la habari la Ufaransa AFP wameripoti Benzema amekamatwa na polisi kwa kesi hiyo hiyo ya Blackmail.
AFP wameripoti kwamba Benzema alienda polisi leo asubuhi saa 3, kabla ya kuwekwa kizuizini.
Endapo atakutwa na hatia basi mchezaji huyo atafunguliwa kesi inayoweza kumuweka ndani kwa miaka 5
Tags
MICHEZO KITAIFA
