
Dar es Salaam Tanzania
Kufuatana na nia thabiti ya Mhe. Rais Jakaya M. Kikwete kuhamasisha kizazi kijacho cha vijana wa Kitanzania; kuanzia tarehe 9 Novemba kwa mara ya kwanza vijana wa kiume wa Kitanzania watapata fursa ya kushiriki katika programu ya mafunzo ya vijana wenye vipaji vya mpira katika kituo hiki chenye michezo mbalimbali.
Kuanzia siku ya Jumatatu ya tarehe 9 Novemba. Vijana wa kiume wa kitanzania waliozaliwa kati ya mwaka 2004 na 2005 wataweza kupata mafunzo ya ukocha kutoka kwa wakufunzi waliopata mafunzo maalum. Zoezi hili litafanyika kuanzia saa 9 mchana hadi saa 12 jioni kwa kila Jumatatu na Ijumaa.
Mafunzo haya yatafanyika kupitia Programu ya Shule ya Soka ya Kituo cha Michezo JMK na yatalenga katika kuongeza vipaji vya mpira vya vijana wa kitanzania. Wale waliozaliwa mwaka 2005 watafanya mazoezi kuanzia saa 9 Mchana hadi saa 10:30 jioni na wale waliozaliwa mwaka 2004 watafanya mazoezi kuanzia saa 10:30 hadi saa 12 jioni.
“Ufanyaji kazi kwa karibu na Timu ya Soka ya Sunderland inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza; utaiwezesha hii shule ya Soka kuwa fursa nzuri kwa vijana wadogo wa Dar es Salaam kupata mafunzo ya kitaalam,” alisema Mkurugenzi wa Mafunzo wa Kituo cha Michezo JMK na Kocha wa zamani wa timu ya Mpira ya vijana Ndugu Ray Power.
Hakutakuwepo mchujo maalum ili kuweza kushiriki katika shule ya soka. Hata hivyo kila kipindi cha mazoezi kinaweza kuhusisha si zaidi ya Wachezaji 60 na Vijana wa Kitanzania wanaotafuta nafasi ya kushiriki lazima watoe uthibitisho wa umri wao.
“Tumenuia kufanya kazi na kukuza vijana wengi kadri itakavyowezekana ambao hawajafikia umri wa miaka 12 wanaoishi Dar. Kipindi hiki cha Ukuuaji kabla ya kubalehe ni muhimu sana katika ukuzaji wa ufundi. Tunalenga kukuza hawa vijana na kuwaunga mkono katika yale wanayoyafanya mitaani na katika timu zao za huko watokako.
Kuelekea mwisho wa Novemba na Mwanzoni wa Mwezi wa Disemba, Wachezaji wakubwa wa Kitanzania waliozaliwa kati ya mwaka 2000 na 2003, wataweza kushiriki majaribio ya kupata nafasi ya kushiriki katika Shule ya Soka ya vijana wenye vipaji katika Kituo cha Michezo JMK itakayofunguliwa Januari Mwaka 2016. Hii shule itakuwa na programu maalum iliyobuniwa na Timu ya Soka ya Sunderland itakayosisitiza mafunzo ya kina na matayarisho ya mechi.
Majaribio
Tarehe za Majaribio ya Kujiunga na Shule ya Soka ya Vijana wenye vijana zitakuwa kama ifuatavyo:
- Jumatatu tarehe 23 na tarehe 30 Novemba; Tarehe 7 Disemba- Wachezaji waliozaliwa Mwaka 2000
- Jumanne tarehe 24 Novemba; Tarehe 1, 8 Disemba- Wachezaji waliozaliwa mwaka 2001.
- Jumatano tarehe 25 Novemba; Tarehe 2 Disemba na Ijumaa tarehe 11 Disemba- Wachezaji waliozaliwa mwaka 2002.
- Alhamisi tarehe 26 Novemba; Tarehe 3, 10 Disemba- Wachezaji waliozaliwa mwaka 2003.

Kituo cha Vijana cha Michezo kilifunguliwa rasmi tarehe 19 Oktoba 2015. Kituo hiki chenye michezo mbalimbali kilijengwa na Symbion Plower ambacho ni kituo cha Kimarekani kinachojitegemea kinachojihusisha na uzalishaji umeme chenye mahusiano ya karibu na Tanzania; Timu ya Soka ya Sunderland kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Marekani; NBA.
Kituo hiki kina kiwanja kamili cha Soka, Viwanja viwili vya kucheza wachezaji watano watano kila upande, Kiwanja cha Mchanga, Viwanja viwili vya Mpira wa Kikapu na taa zenye mwanga mkali zinazowezesha Wananchi kufurahia huduma zipatikanazo kwenye hiki kituo nyakati za jioni.
Kwa maelezo zaidi au maswali, tafadhali wasiliana na Ndugu Adi Raval wa Symbion Power kupitia adi.raval@jmkpark.org na Ndugu Ray Power wa JMK Park kupitia ray.power@jmkpark.org
Ili kupata habari mpya zihusuzo kituo tafadhali wasiliana nasi kupitia Twitter @jmkpark. na Instagram @jmk_park.
Tags
MICHEZO KITAIFA


