Kie Mlay (kulia) kutoka Maryland akiongea jambo na Bwn, Frederick Kanga wakati wa usaili wa kujaribu kuwaoatia Diapora nafasi za kazi kwenye Benki ya Exim yenye makao makuu yake jijini Da es Salaam siku ya Jumamosi Novemba 7, 2015 katika hotel ya Hilton katikati ya jiji la New York..
Kulia ni Peter Mgema kutoka Texas akifanyiwa usaili na Bwn. Frederick Kanga na Dinesh Arora (kulia) ambaye ni Chief Executive Officer wa Exim Bank siku ya Jumamosi Novemba 7, 2015 katika hotel ya Hilton katikati ya jiji la New York
Exim
Bank ya Tanzania siku ya Jumamosi ilifanya usaili kwa Diaspora
Watanzania wanaoishi nchini Marekani jijini New York kwa ajili ya kuwapa
kipaumbele Diaspora na hatimaye kuwapatia kazi kwenye Benki hiyo yenye
makao makuu yake Dar es Salaam, Tanzania.
Akiongea na Vijimambo/Kwanza Production mkuu wa human resources Bwn. Fredirick Kanga alisema sababu kubwa ya Benki hiyo kuwafanyia usaili Diaspora ni kutambua mchango wao na mfumo wa uchapa kazi waliouzoea ili waweze kuutumia nyumbani katika kuleta maendeleo yenye ufanisi katika sekta mbalimbali kwenye Benki hiyo ambayo kazi kubwa ni kutoa huduma bora kwa wateja wake.
Bwn. Fredirick Kanga akijibu swali ni kwanini wasitafute wafanyakazi waliopo Tanzania ambao wengi wao wamemaliza masomo ya juu na hawana kazi. Bwn. Kanga alisema sababu kubwa ya kuja Diaspora nikutokana na kutambua mchango mkubwa wa Diaspora na ufanisi wao katika kazi na sio kweli kwamba hatuajili Watanzania waliopo nyumbani, tunachojaribu ni kuchanganya ujuzi wa Diaspora na nyumbani ili kufanikisha na hatimae kutoa huduma bora na zenye ufanisi mkubwa, huku akisema Benki ya Exim ndio Benki yenye asilimia ndogo ya makato kwenye akaunti za wateja wao nchini Tanzania.
Bwn. Kanga alisema tangia tuanze kuasaili Diaspora tumeisha wapatia kazi wapatao 25 na mwaka jana pekee tuliwapatia nafasi Diapora 6 toka Uingereza na 3 kutoka nchini Marekani.

Baadhi
ya Diaspora wanapenda kurudi nyumbani lakini wanahofia jinsi gani ya
kuanza maisha yao mapya baada ya kukaa ughaibuni kwa muda mrefu. Exim
Benki imeliangalia hilo na ndio sababu kubwa inayowafanya kufanya usaili
kwa WanaDiaspora anaporudi nyumbani anauhakika na kazi yake.
Tags
BIASHARA