Balozi
wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani
Sebregondi (kulia) akibadilishana hati na Mratibu wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba
wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
JUMUIYA ya Ulaya (EU) imetiliana saini na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini yanayofanya kazi kama shirika moja (One UN), ruzuku Euro 200,000 sawa na sh. Milioni 478.
Utilianaji saini huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya UN nchini , Alvaro Rodriguez na Balozi wa EU, Filiberto Sebregondi.
Sebregondi alisema Tanzania imefanikiwa kutengeneza mfano wa namna bora Mashirika ya UN yanavyoweza kufanyakazi kama taasisi moja katika kuboresha maisha ya watu.
Naye Rodriguez, alisema fedha hizo zimelenga kusaidia miradi ya pamoja ya EU NA UN ya mawasiliano, uragibishi, uimarishaji wa ufuatiliaji na uwazi.
Rodriguez, alisema msaada huo ni muhimu katika ufanisi wa maendeleo kwa Tanzania wakati nchi inajipanga kutekeleza malengo ya endelevu SDGs.
“Nchi ina Rais mpya na inahitaji kuwa ya kipato cha kati sisi UN na washirika wetu ni vyema tukaunga jitihada hizi ili kusiwepo na mtanzania atakayeachwa nyuma katika mchakato wa maendeleo,” alisema.
| Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla hiyo. |
| Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez akizungumza katika
hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa
Mataifa Euro 200,000. |
Na Mwandishi Wetu
JUMUIYA ya Ulaya (EU) imetiliana saini na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini yanayofanya kazi kama shirika moja (One UN), ruzuku Euro 200,000 sawa na sh. Milioni 478.
Utilianaji saini huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya UN nchini , Alvaro Rodriguez na Balozi wa EU, Filiberto Sebregondi.
Sebregondi alisema Tanzania imefanikiwa kutengeneza mfano wa namna bora Mashirika ya UN yanavyoweza kufanyakazi kama taasisi moja katika kuboresha maisha ya watu.
Naye Rodriguez, alisema fedha hizo zimelenga kusaidia miradi ya pamoja ya EU NA UN ya mawasiliano, uragibishi, uimarishaji wa ufuatiliaji na uwazi.
Rodriguez, alisema msaada huo ni muhimu katika ufanisi wa maendeleo kwa Tanzania wakati nchi inajipanga kutekeleza malengo ya endelevu SDGs.
“Nchi ina Rais mpya na inahitaji kuwa ya kipato cha kati sisi UN na washirika wetu ni vyema tukaunga jitihada hizi ili kusiwepo na mtanzania atakayeachwa nyuma katika mchakato wa maendeleo,” alisema.
Tags
HABARI KITAIFA