Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi
(kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Serikali la
LUKEMA Community Development and Training Services baadhi ya vibao
maalumu kwa ajili ya kujifunzia wanafunzi wa darasa la awali.Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kulia) akiwagawia madaftari wanafunzi wa darasa la awali ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa kukisaidia kituo hicho. Vifaa vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL kwa kituo cha LUKEMA ni pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina mbalimbali ya wanafunzi wa awali, mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa pili kulia) akimkabidhi baadhi ya mikeka Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Serikali la LUKEMA Community Development and Training Services vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la awali la kituo hicho kama msaada.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (anayeandika ubaoni) akiwachemsha bongo wanafunzi wa darasa la awali wa kituo cha LUKEMA kwa maswali ya hesabu kabla ya kukabidhi misaada ya vifaa vya masomo leo shuleni hapo.
Muonekano wa darasa hilo la awali baada ya kukabidhiwa misaada ya mikeka ya kukalia. Vifaa
vingine vilivyotolewa kama msaada na TTCL kwa kituo cha LUKEMA ni
pamoja na maboksi ya chaki, vibao vya kuandikia, madaftari aina
mbalimbali ya wanafunzi wa awali, mikeka kwa ajili ya kukalia wanafunzi.
Tags
ELIMU








