Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mh. Idd Ramadhan Mapuri
(katikati) akizindua taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na
Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia
Tanzania. kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala Bora Bi. Mary Massay na (kulia) ni mmoja wa wajumbe
walioshiriki kuandaa ripoti hiyo, kutoka nchini Kenya katika taasisi ya
ACHPR, Dk. Naomi Kipuri.
(Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
(Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[DAR
ES SALAAM-TANZANIA] Jamii ya watu wa asili na makundi yao wameiomba
Serikali ya Tanzania kutambua uwepo wao hapa nchini ikiwemo kuwatangaza
kwa mema na kuwasaidia kwa misingi ya haki, hutu na kimaendeleo kama
watu wengine wanaotambulika ndani na nje ya mipaka yao.
Hayo
yameelezwa mapema leo jijini hapa wakati wa uzinduzi wa taarifa ya Tume
ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za
watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania wakiwemo makabila ya
Wa-Akiye,Wa- Hadzabe,Wa- IIparakuyio Masai na wengine wengi.
Akielezea katika uzinduzi huo mmoja wa wajumbe walioandaa taarifa ya
Tume hiyo, ambaye anatoka nchini Kenya, katika taasisi ya African
Commission on Human and Peoples Rights (ACHPR), Dk. Naomi Kipuri
amebainisha kuwa jamii ya watu asilia wamekuwa na kilio cha muda mrefu
cha kutaka kupata haki zao zao msingi na kutambulika zaidi.
“Utafiti
tuliofanya jamii ya watu asilia wamekuwa katika malalamiko ya muda
mrefu ikiwemo kutaka haki zao za msingi. Ikiwemo masuala ya elimu,
makazi na haki zingine. Pia wameomba Serikali kuwatangaza watu hawa wa
asilia ili wasionekane wageni kwani jamii nyingi bado hazijawatambua na
hata kupelekea kuwavunjia hutu wao” alieleza Dk. Naomi.
Aidha,
Dk. Naomi katika uwakilishi wake wa mada kwenye mkutano huo amelezea
namna ya jamii inavyoendelea kuwaona watu hao ni tofauti kiasi cha
kupelekea watu hao kudumaa na maisha yale yale ya asilia.
![]() |
| Dk. Naomi Kipuri wa taasisi ya ACHPR, ya nchini Kenya akijadiliana jambo na Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Tumaini-Makumira, Bw. Elifuraha Laltaika. |
![]() |
| Mmoja wa washiriki wa mkutano huo Mhifadhi Mkuu, kutoka ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Seleman Kisimbo akichangia mada juu ya hali iliyopo sasa ikiwemo jamii hiyo ya watu asilia na changamoto za Mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo suala la ukame inayowakabili katika maisha yao ya vijijini. |
Tags
HABARI KITAIFA




